LABEL ZIKIWA NA USHINDANI NI NJIA NZURI KUPELEKA WASANII WENGI SOKO LA...

LABEL ZIKIWA NA USHINDANI NI NJIA NZURI KUPELEKA WASANII WENGI SOKO LA KIMATAIFA

0

87d24075-c876-47f1-b58e-23fa4f3bedb6LABEL ZIKIWA NA USHINDANI NI NJIA NZURI KUPELEKA WASANII
WENGI SOKO LA KIMATAIFA
Toka mwaka 2016 umeanza soko la muziki wa Tanzania
limeonekana kuzidi kujikita kimataifa zaidi ukiachana na Diamond, Vanessa Mdee,
Ommy Dimpoz, AY,Ali Kiba,Navy Kenzo na Shetta ambao  kwa kiasi Fulani washatoboa ile ozone layer
na kwenda nje kimuziki sasa kumeibuka suala la wasanii kuwasaini WASANII
wengine.

 Kwenye label zao mfano DIAMOND na WCB, tukamsikia OMMY DIMPOZ  akimtambulisha msanii mwingine toka LABEL
yake wakuitwa NEDY MUSIC siku moja baadae tukawasikia NAVY KENZO wakitambulisha
THE INDUSTRY kama label yao ya muziki nao wakatangaza wasanii wao ambao
watakuwa chini yao.

 Ukiangalia wasanii
wote ambao ni wamiliki wa label hizi ni wasanii waliotoboa kimataifa, wanajua A
mpaka Z za za muziki wa kimataifa hii itakuwa rahisi sana kwa wasanii walioko
chini ya label hizi kutoka kimataifa maana wamekaa karibu na nyuki so ni rahisi
kuonja asali, kikubwa ni kujitambua tu, Tumeona THE INDUSTRY wameanza vizuri kwa kichupa kikali cha msanii wa label yao SELINE, tumeona PKP nao wametoa kichupa kikali cha NEDY MUSIC.

Sina shaka na WCB kwani nao HARMONIZE na RAYVANNY vichupa vyao viko poa so kama ni msanii chipukizi na unataka njia yako ya kuelekea kimataifa karibia kwenye mizinga ili atleast uone asali inafanana vipi, na ukionja utamu wake uwe tayari na experience ya kujua mambo yanavyokwenda. nafikiri ushindani uendelee na tusiponde kabisa kuhusu wanaoanzisha LABEL bali tuwasapoti, maana TANZANIA bana kuna watu wanaona suala la label kama wanaigana ila si kweli wenzetu wote duniani suala la label lipo na ni suala serious sana.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY