ZIFAHAMU COLLABO 3 ZA FID Q ANAZOZIKUBALI ZAIDI

ZIFAHAMU COLLABO 3 ZA FID Q ANAZOZIKUBALI ZAIDI

0
 AKIONGEA kwenye kipindi cha So So Fresh cha Clouds Fm kinachoongozwa Baba Jonii AD Plus Adam Mchomvu na MAMY BABY fid q alitaja ngoma zifuatazo kama COLLABO ZAKE TATU ANAZOZIKUBALI ZAIDI

1. UMBO  NAMBA NANE – DAZ BABA  feat FID Q
FID Q alisema wimbo huu kwake unabaki kwenye historia yake kwani ulimfanya akubalike kwa kina DADA, Aliongeza kwa kusema waliutoa kipindi ambacho kulikuwa na maashindano ya mamiss, na alibahatika kupiga show moja ya miss UPANGA, Katikashow hiyo MC alikuwa marehemu Amina Chifupa na alionyesha kumkubali sana FID Q kwani alimfata na kumwambia.
.

2. CHAGUA MOJA –  FID Q feat TID, LANGA, BLACK RHINO, & ADILI
Kumbe chagua moja ulikuwa ni wimbo uliorekodiwa mwanzo pale kwa baucha, kabla ya producer wa fidq.com Castro kupata matatizo na kufungwa jela, hivyo FID Q alitafutwa na P FUNK na kuambiwa kufanya naye ngoma, kwenye FID Q. COM ya mwanzo mpaka RADO alikuwemo lakini walipofanya hii ya pili ilibidi FID Q amwondoe RADO kwakuwa walikuwa wengi na hapo ndipo yalipozuka ya USIULIZE na kuwa bifu kubwa kwa kipindi kile kati ya FID Q na RADO maswahiba hawa wa zamani kipindi wanasoma inasemekana walisoma darasa moja.

3. NENO – FID Q & LORD EYEZ
 FID Q anasema hii nayo ni moja kati ya collabo zake kali, anadai kipindi hiko alikuwa ARUSHA akapigiwa simu na LORD EYEZ , fid anaamini LORD ndo king wa arusha so alipoambiwa kuna mdundo upo kwa Samtimber hakuwa na mashaka nao na alipofika studio walifanya kilichotakiwa na ngoma kutoka, kabla ya story kuja kuwa Beat ya wimo huu inafanana na ya G UNIT, FID Q alisema beat sio kwamba niya G UNIT ila TEMPLATE ZA KEYBOARD ndizo zilizofanana ila sema  wabongo tunabahati mbaya kama mrembo mwenye mapengo
 

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY