DEMO
BASATA YAUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO

BASATA YAUFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO

0

nay wa mitego pale kati patamu

Baraza ka Sanaa nchini (BASATA) limeufungia wimbo wa mwanamuziki Nay wa Mitego unaokwenda kwa jina la Pale kati Patamu kwa maelezo kuwa wimbo huo kwa kiasi kikubwa umekiuka maadili ya sanaa na jamii kwa ujumla.
Nay wa Mitego imeelezwa kuwa amekuwa akitoa nyimbo na kufanya matamasha ya muziki ambayo si kwamba ni kinyume na maadili ya Tanzania lakini pia amekuwa akiwadhailisha wanawake kwa picha anazopiga na maneno anayoyaumia katika nyimbo zake.
Nay wa Mitego hivi karibuni emetoa wimbo wake wa Pale Kati patamu ambao picha za wimbo huu zimesambaa mitandaoni zikionyesha wasichana waliopiga picha wakiwa utupu kitu ambacho si sawa.
BASATA limewakumbusha wasanii wote nchini kufanya kazi kufuatana na taratibu zilizopo lakini pia kuangalia maadali ya nchi ili kuhakikisha kuwa mikwaruzano isiyokuwa yalazima inaepukika na kunakua na ushirikiano wa kuinua tasnia nzima ya sanaa nchini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY