BEI YA MAFUTA YAPANDA, FAHAMU KIWANGO CHA FEDHA KILICHOONGEZEKA

BEI YA MAFUTA YAPANDA, FAHAMU KIWANGO CHA FEDHA KILICHOONGEZEKA

0
Bei ya mafuta imepanda kuanzia leo na kufikia kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kufikiwa tangu Januari.
 Bei mpya elekezi zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) zinaonyesha kuwa dizeli imeongezeka kwa Sh88 kwa lita ikifuatiwa na mafuta ya taa kwa Sh80 kwa lita wakati petroli ikiongezeka kwa Sh23.
 Taarifa ya Ewura imesema kuanzia leo, wakazi wa Dar es Salaam watakuwa  wakinunua petroli kwa bei isiyozidi Sh1,888,  dizeli Sh1,720 na mafuta ya taa Sh1,687 kwa lita.
CHANZO: MWANANCHI

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY