Loading...
FAHAMU SIMBA INAKWENDA WAPI KUWEKA KAMBI KUJIANDAA NA LIGI KUU NA RATIBA...

FAHAMU SIMBA INAKWENDA WAPI KUWEKA KAMBI KUJIANDAA NA LIGI KUU NA RATIBA NYINGINE

0

SIMBA SC inatarajiwa kuondoka mjini Dar es Salaam keshokutwa kwenda Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambao utanatarajiwa kuanza kuanzia Agosti 20, mwaka huu.
Na baada ya maandalizi mazuri ya takriban mwezi mzima, Simba imeialika klabu bingwa ya Kenya, Gor Mahia kwa ajili ya kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki katika Tamasha la Simba Day, Agosti 8.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana, Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva alisema kwamba uongozi wa timu hiyo uliamua kuahirisha programu ya mazoezi iliyopangwa kuanza jana mjini Dar es Salaam kwa ajili ya kupisha sherehe za Sikukuu ya Eid El Fitri.

Source: Bin Zubeir

Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY