FAHAMU YANGA ITAENDA WAPI KUWEKA KAMBI KABLA YA MECHI NA MEDEAMA YA...

FAHAMU YANGA ITAENDA WAPI KUWEKA KAMBI KABLA YA MECHI NA MEDEAMA YA GHANA

0

YANGA SC inatarajiwa kuondoka Ijumaa mjini Dar es Salaam kwenda kisiwani Pemba kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wake wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana Julai 16, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inahitaji ushindi wa kwanza katika mechi za kundi hilo, baada ya kufungwa 1-0 mara mbili dhidi ya MO Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC mjini Dar es Salaam Juni 28, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Hans van der Pluijm amesema kuhusiana na maandalizi yake kuelekea mchezo dhidi ya Medeama anahitaji ushindi tu.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY