Loading...
HARMONIZE – MATATIZO (LYRICS/ MASHAIRI/MISTARI)

HARMONIZE – MATATIZO (LYRICS/ MASHAIRI/MISTARI)

1

VERSE 1
Alfajiri imefika, angaa inang’aa/
Mvua inaanza katika,Ghafla tumbo la njaa/
Naweka sauti kwa spika, Nipate Umbeya wa Dar/
Mara simu inaitaa, jina la anko Twaa/ akisemaa
Mama yu hoi kitandani, kama sio wa leo wa Kesho/
Na kupona sidhani, upate japo neno la mwisho/

KIBWAGIZO

Mi ndo mtoto wake Kee, Nyumbani wananitegemea/
Mdogo wangu wa kike, hali duni alishagaolewa/
Tizama jasho langu la mnyonge, kipato hakikidhi mahitaji/
Napiga moyo konde, Yalabi mola ndo mpaji/

KORASI

MATATIZO

MATATIZO yatakwisha lini , Matatizo kila siku mimi.
MATATIZO yatakwisha lini ,Japo likizo  nifurahi na mimi.

VERSE 2
Mola aliniumba na subira imani pekee ngao yangu/
Mbona nishasali sana ila mambo bado tafarani/
MAMA kanifunza kikabila nikonde sana haini yangu/
tena nijitume sana na vya watu nisivitamani/
Hata mpenzi niliyenaye najua siku atanikimbia, itanitesa ye ndo nguzo/
zile ngoja kesho baadae atazichoka kuzivumilia, anakosa hata matunzo/
nadaiwa kodi nilipopanga, nashinda road nikiranda, nshapiga hodi kwa waganga, kwakuhisi narogwa./
Nikauza maji na karanga, nikawa dobi kwa viwanda, ila kote zero ni majanga, mtindo mmoja./

KIBWAGIZO
Mi ndo mtoto wake Kee, Nyumbani wananitegemea/
Mdogo wangu wa kike, hali duni alishagaolewa/
Tizama jasho langu la mnyonge, kipato hakikidhi mahitaji/
Napiga moyo konde, Yalabi mola ndo mpaji/

KORASI
MATATIZO

MATATIZO yatakwisha lini , Matatizo kila siku mimi.
MATATIZO yatakwisha lini ,Japo likizo  nifurahi na mimi. *2

Lyrics Mashairi yameandaliwa na kuandikwa na Sharo Gangstar wa Kwata Unit.
Instagram Follow me @SharoGangstar_Genius

Loading...

1 COMMENT

LEAVE A REPLY