DEMO
DEMO
HAWA NDIYO WANAOWANIA TUZO ZA LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA

HAWA NDIYO WANAOWANIA TUZO ZA LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA

0

9

Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.
Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Tuzo hizo ni
 • Mabingwa
 • Makamu bingwa
 • Mshindi wa tatu
 • Mshindi wa nne
 • Timu yenye nidhamu
 • Mfungaji bora
 • Mchezaji bora wa Ligi
 • Kipa bora
 • Kocha bora,
 • Mchezaji bora chipukizi
 • Mchezaji bora wa kigeni
 • Goli bora la msimu na
 • Mwamuzi bora.
Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo;-
Mchezaji bora wa Ligi
 • Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar),
 • Juma Abdul (Yanga) na
 • Mohamed Hussein (Simba)
Kipa bora
 • Aishi Manula (Azam),
 • Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na
 • Deogratius Munishi (Yanga).
Kocha bora
 • Hans Van Pluijm (Yanga),
 • Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na
 • Salum Mayanga (Tanzania Prisons).
Mchezaji bora chipukizi
 • Farid Mussa (Azam),
 • Mohamed Hussein (Simba),
 • Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na
 • Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).
Mchezaji bora wa kigeni
 • Donald Ngoma (Yanga),
 • Thabani Kamusoko (Yanga) na
 • Vincent Agban (Simba).
Waamuzi bora
 • Anthony Kayombo,
 • Ngole Mwangole na
 • Rajab Mrope.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY