DEMO
LIST YA WASANII NA DJ TOKA TANZANIA WALIOTAJWA KUWANIA TUZO ZA...

LIST YA WASANII NA DJ TOKA TANZANIA WALIOTAJWA KUWANIA TUZO ZA AEAUSA(MAREKANI) 2016

0
9Wanamuziki na DJ kutoka Tanzania ambao ni Diamond Platnumz, AY, Alikiba, Joh Makini na DJ D-Ommy, Ommy Dimpoz, Raymond, Harmonize wote wametajwa katika vipengele tofauti kuwania tuzo za Afrika Entertainment Awards, za nchini Marekani.
Mgawanyiko wa vipengele uko hivi kwa kila msanii, Diamond ametajwa kuwani tuzo ya Best Male Single, Best Video of The Year, pamoja na People’s Choice, AY na Alikiba wanawania kipengele cha Best Collaboration kwa wimbo Zigo Remix (AY) na Nagharamia (Ali Kiba).
Rapper Joh Makini ametwajwa kuwania Best Hip hop Artist na Best Video of the Year kwa wimbo wake Don’t Bother, huku Ommy Dimpozi akiwani kipengele hicho hicho kwa wimbo wake wa Achia Body.
Mlimbwende Vanessa Mdee ametajwa katika kipengele cha Best Female Single kwa wimbo wake Never Ever, Linah kipengele cha Best Female Artist, Yamoto Band  kwenye kipengele cha Hottest Group.
Harmonize ametajwa kuwani kipengele cha Best New Artist wakati Raymond akitajwa kwenye kipengele cha Best New Talent.
Dj pekee kutoka Tanzania ni DJ D-Ommy wa Clouds FM aliyetajwa kuwania kipengele cha Best DJ na wa mwisho ni Millard Ayo akitajwa kuwania kipengele cha Best Blogger.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY