Loading...
Mahakama ya Mafisadi Kuanza hivi karibuni

Mahakama ya Mafisadi Kuanza hivi karibuni

0


Dar es Salaam. Mahakama ya Mafisadi inayotarajiwa kuanza hivi karibuni, itaanza na mzigo wa kesi zilizopo kuendeshwa kwa kusuasua.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Televisheni ya Clouds jana, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe alisema kuna kesi 176 za uhujumu uchumi tangu Juni mwaka jana.

Pia, Dk Mwakyembe alisema kesi 13 zimekamilika, watu 12 wamehukumiwa vifungo vya jela na wanawadaiwa Sh29 bilioni.

“Nchi ilipofikia tunataka tuachane na hizi tabia za udokozi, unapopewa mamlaka ya kuhudumia umma,” alisema.

Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY