mamba 100 watoroka hifadhini baada ya mafuriko

mamba 100 watoroka hifadhini baada ya mafuriko

0

Image copyrightGETTYImage captionUchina inatafuta mamba 100 waliotoroka kutoka kwenye hifadhi moja baada ya mafuriko makubwa

Mamlaka nchini Uchina inajaribu kutafuta takriban mamba 100 waliotoroka kutoka kwenye hifadhi moja baada ya mafuriko makubwa yanayoshuhudiwa nchini humo.
Mafuriko hayo yaliwawezesha mamba hao kuogelea na kuondoka kwenye eneo lilizingirwa kwenye hifadhi hiyo katika mkoa wa Anhui.

Image copyrightREUTERSImage captionTakriban watu 180 wamekufa maji kutokana na mafuriko hayo makubwa

Ni nadra sana kupata Mamba hao wa Uchina mwituni.
Hata hivyo mamba huwindwa kutokana na ngozi yao inayouzwa kwa bei ghali mno pamoja na nyama yao na pia hutumika kuwaburudisha watalii.

Image copyrightTHINKSTOCKImage captionNi nadra sana kupata Mamba hao wa Uchina mwituni.

Takriban watu 180 wamekufa maji kutokana na mafuriko hayo makubwa yanayoendelea kushuhudiwa nchini China.
Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kutorokea maeneo yenye milima ilikutoroka mafuriko yanayochacha.
bbc

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY