Loading...
MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU GARI AINA YA LAMBORGHINI

MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU GARI AINA YA LAMBORGHINI

0
Image of Lamborghini

1.Lamborghini ni jina la mwanzilishi wa kampuni hiyo aliyekuwa anaitwa Ferruccio Lamborgini.

2.Lamborghini yenye mwendokasi zaidi duniani inaitwa (Murcielago R-GT) na mwendo wake ni Kilomita 370 kwa saa.

3.Mwaka 1963 ndiyo mwaka ambao Lamborghini iligunduliwa kabla walikuwa wakizalisha matrekta tu.

4.Lamborghini yenye thamani zaidi duniani ni Lamborghini Reventon inauzwa zaidi ya Shilingi bilioni 3.2 kwa Lamborghini moja.

5.Magari mengi aina ya Lamborghini yaliitwa majina baada ya Waasisi kutoka Uhispania.

6.Lamborghini ya kwanza ilikuwa inaitwa Lamborghini 350GTV mwaka 1963.

7.Mwanzoni kampuni ya Lamborghini ilikuwa ni kampuni huru ila kwasasa inamilikiwa na Volkswagen AG wakishirikiana na Audi.

8.Magari mengi aina ya Lamborghini yana Engine aina ya V 12 kasoro Gallardo ambayo yana V10.

9.Mmiliki wa Lamborghini mwanzoni alikuwa anaendesha Ferrari ila gari lake lilikuwa na matatizo mengi sana hasa Clutch, hali iliyomuudhi na kusababisha kuanza kutengeneza magari na kuachana na Kutengeneza Ma Trekta.

10.Mwaka 2007 Lamborghini waliuza magari 2580 kiwango kikubwa zaidi ambacho waliwahi kuuza kwa mwaka.


Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY