MAN WALTER SASA AWAKARIBISHA WATU WA BAND STUDIO KWAKE BAADA YA KUKAMILISHA...

MAN WALTER SASA AWAKARIBISHA WATU WA BAND STUDIO KWAKE BAADA YA KUKAMILISHA HILI

0

Producer Man Walter moja kati ya Producer aliyejipatia umaarufu sana mara baada ya kutengeneza nyimbo zilileta Tuzo 5 kwenye tuzo za kili wakati huo huo yeye mwenyewe akakosa tuzo kama Mtayarishaji bora wa mwaka, hali iliyofanya watu wamuongelee sana na kusababisha mwaka uliofuatia kupata tuzo.

Man Walter amewakaribisha watu wa BAND baada ya kukamilisha vifaa rafiki kwa muziki wa live, Man Walter akiongea kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio alisema Studio yake kwasasa inavifaa vipya kwa ajili ya watu wa BAND, anadai mwanzo ilikuwa ni kama asilimia 60 tu ila kwasasa vifaa vilivyopo kwa watu wa Band wanaweza wakarekodi vizuri tofauti na mwanzo na anakadiria imekamilika kwa asilimia 90.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY