Loading...
MAVITU YA WINGA MPYA SIMBA YAWATISHA YANGA

MAVITU YA WINGA MPYA SIMBA YAWATISHA YANGA

0

YANGA wamepata habari za mavitu anayofanya winga mpya wa Simba, Shiza Kichuya wakatishika lakini wakaishia kubeza, lakini wenzao wa Msimbazi wakawaambia kwamba subirini mtatuelewa tu.

Kichuya amekuwa miongoni mwa wachezaji waliopata bahati ya kuanzia mguu mzuri Simba na amekuwa kipenzi hata cha viongozi wanaoibuka mazoezini. Ukifika kushuhudia mazoezi ya Simba winga, Kichuya kutokana na kiwango cha juu anachokionyesha kocha Joseph Omog amempigia tiki ndefu na kumwambia ‘excellent’ neno ambalo kwa mara ya mwisho alilisikia akiwa kidato cha nne.

Kocha Omog ambaye yuko wazi katika kukosoa na kusifu inapombidi alisema Kichuya yuko vizuri kiufundi na atakachomwongezea ni uwezo wa kufikiri yaani acheze kwa akili na nidhamu ya mchezo kulingana na maagizo atakayopewa.

“Kiufundi ni mchezaji mzuri, anashambulia, anachezesha timu, anakaba na mambo mengi kwangu safi, lakini ili awe bora zaidi anatakiwa ajengwe kiakili. Nataka nimtengeneze aweze kufanya kazi na kutimiza majukumu yake kwa akili na nidhamu ya mchezo,” alisema Omog ambaye msingi wa kikosi chake ni nidhamu.

Katika mazoezi ya Simba yanayoendelea kwenye vilima vya Uluguru Uwanja wa Highlands eneo la Bigwa, mjini hapa, Kichuya ameonyesha uwezo wa juu katika kupokea, kutoa pasi na kuchezesha timu.

Mashabiki wanaoshuhudia mazoezi hayo, wamekuwa wakimpigia kelelekila alipogusa mpira kutokana ufundi anaouonyesha. Ni burudani tu, mara kaupokea kwa nyuma, katoa pasi vile, kakaba hivi, ilimradi tu na pamoja na matukio hayo, mipira yake imekuwa na faida kwa timu, siyo kazi bure.

PACHA WA AJIB

Katika mazoezi ya Alhamisi jioni, Kichuya alipangwa kikosi kimoja na Ibrahim Ajib na Danny Lyanga lakini wakiwa mchezoni, Ajib na Kichuya ni kama wameshacheza pamoja kwa kipindi kirefu kwa namna wanavyojuliana.

Kichuya alicheza winga ya kulia na wakati mwingine kushoto, ikipigwa kwa Kichuya, itafika kwa Ajib au Ajib atamrudishia mambo yanakwenda.

mwanaspoti

Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY