Loading...
MFAHAMU STRAIKER MPYA WA “KIMATAIFA” WA SIMBA SC.

MFAHAMU STRAIKER MPYA WA “KIMATAIFA” WA SIMBA SC.

1

Anaitwa Goue Fredric Noel Blagnon, ambaye amezaliwa mwaka 1985.
Ni raia wa Ivory Coast kule wanapotokea mastaa kibao kama Didier Drogba, Kalou, Yaya Toure na Wengine kibao.

Anacheza nafasi ya Ushambuliaji aka Straika.
Sio mchezaji wa kumchukulia poa poa kwani amewahi kukipiga katika moja kati ya club kubwa Afrika ASANTE KOTOKO tokea Ghana.

Kwasasa amejiunga Simba akitokea Club ya Nchini kwao Ivory Coast inaitwa Africa Sports d’abidjan moja kati ya Club ya zamani kwani ilianzishwa mwaka 1947.

Anapenda jezi number 11 ila alipotua Simba alikutana na changamoto ya kupata jezi namba hiyo kwani inavaliwa na Mchezaji Kiongozi Mussa Hassan Mgosi.

Blagnon anaamini jezi namba Kumi na Moja ( 11 ) Ana bahati nayo na hata alipotua Simba alitamani sana kuvaa jezi namba kumi na Moja, ila alipokuta Mr. Captain anavaa hiyo basi alikuwa mpole, na kwasasa inawezekana akawa anavaa jezi namba 9.
                             

Loading...

1 COMMENT

LEAVE A REPLY