Loading...
MFAHAMU VIZURI PENCE, MGOMBEA MWENZA WA DONALD TRUMP

MFAHAMU VIZURI PENCE, MGOMBEA MWENZA WA DONALD TRUMP

0

PenceImage copyrightAPImage captionPence amekuwa gavana wa Indiana tangu 2013

Gavana wa Indiana Mike Pence amechaguliwa kama mgombea mwenza wa Donald Trump anayewania kiti urais kupitia chama cha Republican.
Bw Pence, 57, amekubali nafasi hiyo baada ya kukutana na Trump na familia yake nyumbani kwake Indianapolis .
Wachanganuzi wanasema Trump anatumaini Bw Pence atamsaidia kuwavutia vigogo katika chama chake kwani ni mtu mwenye uzoefu mkuu na anayependwa na wahafidhina katika chama cha Republican.
Aidha, ni mwanachama wa vuguvugu la siasa za mrengo wa kulia la Tea Party.
Bw Pence amehudumu kama Gavana wa Indiana tangu 2013, lakini pia kama mbunge katika Congress kwa miaka 12 na amewahi kushikilia wadhifa wa tatu kutoka juu katika uongozi wa chama chake.

PenceImage copyrightGETTYImage captionTrump atatumai Pence atamsaidia kuwavutia wahafidhina

Wakati mmoja alikusudia kuwania kiti cha urais katika uchaguzi huo wa mwaka huu lakini kisha akaghairi, akilenga kutetea kiti chake katika uchaguzi wa ugavana unaokuja katika jimbo lake.
Hata hivyo siasa za jimboni mwake nazo hazimkalii uzuri katika miaka ya hivi karibuni.
Mbali na kuwa mpinzani wake anaelekea kuzidisha umaarufu wake, pia mwendelezo wa sera za chama chake umemletea changamoto chungu nzima.
Machi mwaka jana aliweka saini sheria ya kuimarisha kuwepo kwa uhuru wa kiabudu lakini makundi ya wanaoendeleza mapenzi ya watu wa jinsia moja, wakamlalamikia kuwa wanabaguliwa katika taasisi zenye misimamo ya kidini.
Alipoifanyia sheria hiyo marekebisho ya kuwaridhisha hao wanaoendeleza mapenzi ya watu wa jinsia moja wanachama wa Republican wakamkashifu wakisema amesaliti maadili ya chama hicho.

PenceImage copyrightAPImage captionAlikuwa amepanga kuwania urais Marekani mwaka huu

Pia sheria aliyoitia saini ya kukataza wanawake kuavya mimba iwapo watagundua mapema mtoto atakayezaliwa atakuwa na ulemavu fulani pia imekuwa ikipingwa vikali.
Bw Pence alilelewa katika familia ya Kikatoliki pamoja na nduguze watano huko Columbus, Indiana.
Japo yuko katika chama cha Republican yeye anasema alipata motisha wa kuingia katika ulingo wa siasa kutoka kwa wanasiasa kama vile John F. Kennedy na Martin Luther King Jr .
Asema walikutana na mkewe Karen, katika kanisa la Kiinjilisti na ndipo misimamo yake ya kisiasa ilipoimarika.
Bw Pence atakuwa makamu wa rais wa Bw Trump iwapo atafanikiwa kumshinda mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton kwenye uchaguzi mkuu Novemba.
bbc
Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY