Mhasibu mkuu polisi Asimamishwa Kazi. Soma kujua sababu

Mhasibu mkuu polisi Asimamishwa Kazi. Soma kujua sababu

0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Taarifa kutoka wizara hiyo zimesema, Msaki alifanya malipo ya Sh305, 820,000 kama posho ya chakula kwa watu ambao siyo askari kuanzia mwaka 2013/2014 hadi 2015/2016.
TAARIFA KAMILI
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Frank Msaki kwa madai ya kufanya malipo hewa ya posho ya chakula kwa watu wasio askari.
Taarifa kutoka wizara hiyo zimesema, Msaki alifanya malipo ya Sh305, 820,000 kama posho ya chakula kwa watu ambao siyo askari kuanzia mwaka 2013/2014 hadi 2015/2016.
“Baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa na ukaguzi Maalumu kufanywa na mkaguzi wa ndani wa Jeshi la Polisi, imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimefanyika ili kuhalalisha malipo hayo hewa,” alisema Rwegasira.
Mwananchi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY