Loading...
MOTO WA MBWANA SAMATTA (GENK) SI WAKITOTO, DE GEA WA MANCHESTER...

MOTO WA MBWANA SAMATTA (GENK) SI WAKITOTO, DE GEA WA MANCHESTER UNITED AJIANDAE

0

Ukiachana kuwa Mbwana Samatta mwaka huu aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuweka historia kwakuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya Mchezaji bora wa afrika anayecheza ligi ya ndani.

Jana pia ameweka historia mbili kubwa, kwanza kuwa mchezaji wa kwanza kucheza michuano ya Europa akiwa na timu yake ya  Genk ya Ubelgiji, Historia nyingine ni ile ya Kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga goli katika michuano ya Europa.

Katika mechi yao ya Jana Genk walishinda kwa bao mbili kwa bila huku Samatta akitupia Goli la pili dakika ya 79, Goal la kwanza la Genk lilifungwa na Kebano kwa mkwaju wa Penalty

Kwasasa Genk ipo katika hatua ya mtoano ili kuingia katika hatua ya makundi ambako huko itakutana na timu kama Manchester United ya Uingereza, Endapo watapangiwa kundi moja Na Man U tusishangae kuona De Gea naye akakutana na balaa la Samatta.

Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY