Loading...
USAJILI : SIMBA YAMNASA MCHEZAJI HUYU WA KIMATAIFA

USAJILI : SIMBA YAMNASA MCHEZAJI HUYU WA KIMATAIFA

0
Club ya soka ya Simba licha ya kuwa inafanya mambo yake ya usajili kwa siri ila  leo imevuja taarifa nyingine kuhusu kumsajili mchezaji wa kimataifa anayetokea nchi ya Zimbabwe anayeitwa Method Mwanjali.
Simba ambayo kwasasa wanafanya mazoezi yao katika chuo cha Ufundi Kurasini, Inasemekana mchezaji huyo kapigiwa pande na Mchezaji mwingine Majadvi ambaye uwezekano wake wa kurudi Bongo kuungana na Simba umekuwa Mgumu.
Kulingana na chanzo chetu cha habari Mwanjali tayari kashatua Tanzania na Kesho anatarajiwa kuanza mazoezi katika timu hiyo ya mitaa ya Msimbazi.
Mwanjali amewahi pia kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika Club ya Mamelody Sundowns na Mpumalanga FC.

Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY