Loading...
TETESI NA HABARI ZA USAJILI LEO JULY 4

TETESI NA HABARI ZA USAJILI LEO JULY 4

0

Manchester United imehusishwa kumsajili Mchezaji wa  raia wa Mexico Hirving Lozano  mara baada ya michuano ya Olympics ambayo itafanyika Brazil. Lozano ameshaichezea timu ya taifa ya Mexico mara 8.

Barcelona inatajwa kumsajili tena mchezaji Denis Suarez ambaye alikuwa Villareal kwa mkopo, Denis Suarez alikuwa ni mchezaji wa Barcelona B toka mwaka 2013 mpaka 2015.

Van Der Wiel Amefanikiwa kusainiwa na timu ya Fenerbahce  ya Uturuki kwa mkataba wa miaka minne (4) kutoka club ya Paris Saint Germany ya Ufaransa.

Juan Mata amekuwa akihusishwa na kusepa ManChester United na kutimkia Everton toka taarifa za ujio wa kocha Jose Mourinho, Everton inatajwa zaidi kwani kuna kocha wake wa zamani wakti Mata akikipiga VALENCIA ya Hispania. Inaelezwa Mata na Mourinho hawaelewani kwani hata wakati MOURINHO yupo Chelsea ndiye aliyemuuza Mata kwa Manchester United.

PSG, Rais wa PSG amesema hawanampango wa kufanya deal ya kumsaini mchezaji wa Real Madrid James Rodriguez, Amekataa kwa kusema hawajafanya mazungumzo na Madrid wala Hawajafanya mazungumzo na James.

Atletico Madrid Imetajwa kumsajili Fernando Torres ambaye alikuwa Atletico kwa mkopo kwa muda wa miezi 18 sawa na mwaka na nusu kutokea AC MILAN ya italy.

Manchester City, Imefanikiwa kupata saini ya Oleksandr Zinchenko kwa mkataba wa miaka 5, Zinchenko ni raia wa Ukrain ambaye ametokea timu ya FC UFA.

Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY