UCHAMBUZI : BABU TALE KUINGIA KWENYE MZOZO NA WASANII INAONYESHA HAJAKOMAA BADO.

UCHAMBUZI : BABU TALE KUINGIA KWENYE MZOZO NA WASANII INAONYESHA HAJAKOMAA BADO.

0

Karibu katika kona hii ya Uchambuzi wa Sharo Gangstar.


Babu Tale ni moja kati ya mameneja ambao nathubutu kusema wanamchango mkubwa sana kwa baadhi ya wasanii ambao wamewahi kuwasimamia, anaujua muziki wa Tanzania Vizuri. Ukisikia Nikki Mbishi kajiunga Tip Top ndani ya miaka miwili huwezi kushangaa kumsikia Nikki Mbishi akiimba kama Shetta au Diamond, Babu Tale hashindwi hili.
Anyway leo sipo kuongelea hilo, BABU TALE mara kadhaa sasa amekuwa akiingia kwenye mzozo na wasanii hasa wanapoonyesha kutoa yao ya moyoni kumhusu yeye, Unaukumbuka mstari wa Baghdad? ule unaosema “Game ishakuwa ya wadau, Tale ananguvu ya Kufanya Media House Wakudharau”  huu ulikuwa mstari wa Baghdad kwenye mtazamo Remix.
Baada ya huu mstari iliripotiwa kuwa Tale aliousikia tu alim’maindi sana Baghdad na kwenye Group la wasanii TALE akawa amemuondoa Baghdad.
Sasa Juzi baada ya Roma kuachia wimbo wake wa KAA TAYARI, kama Unavyomjua Roma akampapasa Tale kwa Mstari ambao ulimlenga wazi Babu TALE kwa kusema ” Meneja Kamganda Dangote Kaisahau TipTop”
baada tu ya Roma kutambulisha wimbo wake East Africa RADIO kupitia kipindi cha Planet Bongo chini ya Mjukuu wa Ambua DULA,Roma anadai kabla hajaupeleka wimbo huo redioni alimsikilizisha Tale na Tale akamwambia AUFUTE mstari huo na kama hataufuta basi wimbo huo hautatoka.
 Babu TALE naye alienda redioni bila kuwa na mwaliko wa redio hiyo na Kuanza kusema kwanza Roma Hajamzidi chochote Tale, Tale alisema kamzidi roma Followers insta, kamzidi mafanikio, mara yeye ndiye meneja mkubwa zaidi afrika, yeye ndiye meneja mwenye mafanikio Afrika.
 Sasa Tale unafikiri  wewe kumzidi Followers Roma Instagram kunabadili ukweli wa mstari alioutoa Roma? Wapenzi wa Tip Top wanataka kumsikia TundaMan, Madee, Dogo Janja Kwenye Redio na sio Safari za kila siku na Diamond.
Huwa nakaa nafikiria Kuhusu RayMond aliyebatizwa mpaka jina la Raymond Tip Top ambaye licha ya kuwa na kipaji cha ajabu ila alikaa miaka mitano (5) bila kutolewa Rasmi wakati huo Tale umeshikilia Madee pekee, Nafikiri Tale unatabia ya kujisahau hasa moja kati ya msanii wako anapokuwa anafanya vizuri wengine unawasahau kabisa.
Kipimo cha mtu kukomaa hakipimwi wakati wa mafanikio bali wakati anapokuwa na changamoto mbalimbali, nachokiona hapa Tale anapenda kusifiwa tu, Ukimpa changamoto anakuchukia na hapendi  Martin Luther King Jr anakwambia  
“The Ultimate measure of a man is not where he stands in a moment of Comfort and Convenience, but where he stands at times of challenge and Controversy.”

Nafikiri kwenye Challenges kama hizi kilikuwa kipindi cha Tale Kutuonyesha kuwa wewe ni meneja wa msanii mkubwa Afrika kwa kujibu kimeneja mkubwa ila Mapokeo yako kwenye hizi ishu za Baghdad na Roma bado ninamashaka na ukomavu wako kwenye Masuala kama haya, na haujarespond  kimeneja mkubwa bali ki local manager.
 
Nakuacha na hili tu Kama unahisi wamekukosea wasamehe maana Mahatma Gandhi  anasema The Weak Can Never Forgive,Forgiveness is the Attribute of the Strong . ila kama ni kweli  mistari wanayoiimba kukuhusu wewe Waonyeshe hawakosahihi kwa kwenda tofauti na maneno yao., na hii itakuwa faida  kwako.
Maoni yako ni muhimu sana. andika hapo chini au kupitia 0672314066

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY