UCHAMBUZI : MAKOMBO YA AZAM YAGEUKA LULU KWA SIMBA

UCHAMBUZI : MAKOMBO YA AZAM YAGEUKA LULU KWA SIMBA

0

Timu ya Azam Imewauza kwa mkopo wachezaji wake wawili kwa mkopo ambao ni AME ALI na Golikipa Mwadini Ali.

Kipa Mwadini Ali ni kipa ambaye msimu wa Ligi ulioisha hakucheza mechi zaidi ya Tatu ligi kuu, alisugua sana Benchi ila Simba bado wameona isiwe Tabu.
Ame Ali naye ni mshambuliaji ambaye hakuwa na Msimu mzuri sana wa Ligi iliyoisha, mara nyingi hakuwa na nafasi katika kikosi cha Kwanza, na hata alipopata nafasi alikuwa akiingia kama Substitution(Mchezaji wa Akiba) ila Kwa Simba Bado amegeuka Lulu.
Wakati Azam ikiwauza Ame Ali na Mwadini Ali wao wanamsajili mchezaji wa Kimataifa tokea Medeama ya Nchini Ghana Enock Atta Agyei kwa mkataba wa miaka miwili.
Mwerevu najua kuna kitu amejifunza, ila Shabiki maandazi asiyependa kuambiwa ukweli najua ataibuka na mapovu yasiyoeleweka ila ukweli utabaki ukweli.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY