UCHAMBUZI : SOKO LA NDANI TAYARI, DAYNA MACHO NA AKILI YAKO VIWAZE...

UCHAMBUZI : SOKO LA NDANI TAYARI, DAYNA MACHO NA AKILI YAKO VIWAZE KIMATAIFA SASA

0


Dayna Nyange mwanamuziki ambaye mimi binafsi nilianza kumsikia kwenye wimbo ” Mafungu Ya Nyanya ” aliomshirikisha Diamond Platnumz wa Kipindi hiko Msanii  Marlaw mzee wa Bembeleza.

Nathubutu kusema toka kipindi hiko Dayna Nyange amekuwa na mwendelezo mzuri sana wa kutoa Hit Songs, Kama Muziki ungekuwa Kikosi cha Timu ya Mpira Dayna kwasasa anastahili awe ndani ya First Eleven.

Amekuwa mwanamuziki mpambanaji kweli kweli, Sijui kuhusu changamoto anazopitia kwenye muziki ila najua zipo tu na ni nyingi maana ni mtoto wa kike huyu ila bado amekuwa Imara anafanya kazi nzuri na watanzania wanazielewa.

Hupaswi sasa kubaki ulipo kila siku ni muda wa ku move on, ni muda wa kukazia kwenye soko la kimataifa, wazungu wanakwambia
” Every day is a new day, and you’ll never be able to find happiness if you don’t move on.”

Nafikiri ni muda sasa wa Dayna kutusua kimataifa, tuanze kuona ngoma zake zikipata Airtime Trace, Mtv na Televisions nyingine za kimataifa. Nafikiri anahitaji kusaidiwa miongozo ya namna nzima kina Vanessa wanafanya mpaka kufika walipo.

Nafikiri lazima kuwe na Connections na hizo Connections lazima kuwepo na watu wa kukukingia kifua anapokuwepo mtu anayejua A na B zako ni tofauti na kutokuwepo kabisa asiyejua chochote kuhusu msanii husika.
Inawezekana pia Dayna ni muoga wa kuthubutu kwa kuamini hawezi ila Nelson Mandela anakwambia ” It always seems impossible until its done. ” 


Jaribu dada yangu mi naamini unaweza kabisa kufika walipo kina fulani fulani, Jipendekeze pendekeze nawewe wakushike mkono, wakuonyeshe njia  maana ukisema upambane nao  wakati wao tayari wapo njiani na wewe unawafatissha kwa nyuma  na wanaijua njia itafika mahali wakupitishe njia ambayo siyo yenyewe then wakupoteze ukishapotea wao wanarudi njia kuu na kuanza kukucheka.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY