Loading...
UCHAMBUZI : UJIO WA SINGELI UTAUA TAARAB NA NI TISHIO KWA BONGO...

UCHAMBUZI : UJIO WA SINGELI UTAUA TAARAB NA NI TISHIO KWA BONGO FLEVA

0

SINGELI KUIUA TAARAB
Ni muziki unaoaminika chanzo chake ni Uswahilini na mwanzo wakati unaanza washabiki wake wengi walikuwa ni watu wa Uswazi.
Waswahili wanasema “mwanzo ni Mgumu”, ila katika kila mwanzo wenye mafanikio basi humfanya muanzishaji wa jambo hilo Kuongeza juhudi maana anakua anaona mbele kuna nini.

SINGELI naweza nikasema ni muziki unaokua kila kukicha ulipo na ulipoanzia sio sawa kuna maendeleo fulani makubwa, Mwanzo ulikuwa ni muziki wa Uswazi kwenye Vigodoro ukapiga hatua mpaka ukaanza kuchezwa kwenye Radio.

Nakumbuka Radio ya kwanza kuanza kuusikia muziki huu ilikuwa EFM, kisha redio nyingine kama East Africa Radio na Clouds Fm kwasasa SINGELI zimeanza kusikika.

Nimewahi kuwa naongea na baadhi ya watu kuwa huu ujio wa Singeli unaweza ukapunguza au kuiua Taarab, Kuna baadhi ya watu wakaniunga mkono wengine wakanipinga, ila Kuna Msemo wazungu wanasema
” Every New Beginning Comes from other Beginning’s end ”  Yani
  ”  Kila jambo Jipya Linalotokea huwa linatokana na Jambo lililokuwepo Kufikia Mwisho ” 
 naweza nikachukua mfano mdogo tu Kwenye kipindi cha Radio cha Leo Tena Cha Clouds Fm huwa wanakipengele cha Kucheza wimbo wa taarab ila siku hizi huwa nyimbo za Singeli nazo zinapata nafasi ya kusikika kwenye nafasi hiyo hiyo.

 Kipindi cha Kwa Raha Zetu nacho ni kipindi Ambacho kwa miaka mingi kinaeleweka ni kipindi cha Taarab ila nacho kimekuwa kinacheza SINGELI.

Kitu kizuri huwa hakihitaji sana Promo, Labda  nikuulize toka Umeanza kumjua Msanii kama Ben Paul ni miaka mingapi? je  umewahi kumuona anapost video akiimba wimbo wa Taarab?  ila Ben Paul na baadhi ya wasanii wameshaonekana wakipost video za Watu wa Singeli tena wakionyesha kuzikubali ngoma zao.

Mapokeo ya muziki huu wa SINGELI yamekuwa tofauti sana, yameonekana kugusa watu wa aina tofauti sana, licha ya kuwa ni muziki ulioanzia ukanda fulani(Pwani) ila umekuwa gumzo mpaka kanda nyingine.

NAFASI YA SINGELI KATIKA BONGO FLEVA
Singeli pia imepenya mpaka ukanda wa Bongo Fleva, siku hizi sio ajabu kumsikia Dj akicheza SINGELI kwenye kipindi kinachopiga Bongo Fleva, wasanii kama Man Fongo na dude lake la Hainga Ushemeji umekuwa unasumbua sana kwenye nyimbo za Bongo Fleva. kwa hili Bongo Fleva hamuoni mmeingiliwa?

Singeli zimeanza mpaka kupata nafasi kwenye Top 20 za Redio kubwa, hili suala Bongo Fleva Haliwatishi?
Juzi kati nimeanza kusikia Tangazo kuhusu Tigo Pesa la Tigo lililopigwa na Msanii wa Singeli, na hili nalo hamuoni Bongo Fleva Haliwatishi?

Kwenye shows chache ambazo zimeshawahusisha wasanii wa Bongo Fleva na Wasanii wa Singeli tayari imeshaanza Kuonekana wasanii wa Singeli wakifanya vizuri kuliko Bongo Fleva.
Siwatishi Bongo Fleva ila nachotaka niwakumbushe ni wazidi kukaza, Kuomgeza Ubunifu, ili kukabiliana na ushindani huu unaokuja kwa kasi, maana  unaambiwa  ” The Best Preparatios for Tomorrow is doing your best Today “ by Jackson Brown.
Imeandikwa na Sharo Gangstar wa Kwata Unit

Loading...

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY