UCHAMBUZI: WASANII NA JUHUDI ZA KUFANYA SHOW ZA FIESTA,LAKINI WANAFELI KWENYE HESABU...

UCHAMBUZI: WASANII NA JUHUDI ZA KUFANYA SHOW ZA FIESTA,LAKINI WANAFELI KWENYE HESABU MUHIMU

0


Karibu tena kwenye Kona Ya Uchambuzi na Sharo Gangstar.

Hakuna ubishi kuwa Fiesta ndiyo show kubwa zaidi Tanzania, Ila ukubwa naouongelea hapa ni kwakuwa ni show Inayokutanisha wasanii wengi kwa pamoja, Promo, na mapokeo yake kiujumla karibu katika kila sehemu ambayo huwa inafanyika.

 Ila sina uhakika  saana katika Ukubwa wa PESA wanayolipwa wasanii kama nayo huwa ni kubwa as we compare ukubwa wa show hii na baadhi ya show za makampuni binafsi kama ya mitandao ya simu na Bia.

Kuna jambo moja  ambalo huwa linanishangaza kwa wasanii wa TANZANIA, huwa nahisi ni ukosefu wa akili ya ziada jambo ambalo linatusababishiaga Jam kwenye muziki wetu, Jam Ambayo siyo ya Lazima.

Imekuwa katabia sasa unakuta msimu wa Fiesta ukikaribia kila msanii kutoa wimbo mpya, Nyimbo nyingine unaona kabisa mtu amekurupuka tu kiasi kwamba anafanya kazi chini ya kiwango chake kisa FIESTA Huu ni Utumwa.

Muda ambao wasanii wanatoa nyimbo mpya, ni muda ambao kiuhalisia ngoma haiwezi Kuhit kihivyo maana ni kipindi ambacho nyimbo zinakuwa nyingi sanaaa, zinazobahatika kupata platform nzuri zinakuwa chache sana TENA mpaka kushikana mikono.

Ndiyo zile mnaenda kwenye Interview  za kazi watu 200 wakati wanaotakiwa ni watu wawili tu, hapo ili kupata nafasi inabidi Uwe bora kweli kweli au Kubebana na kujuana lazima   kuwepo ili kupata nafasi ila pasipo hivyo tusidanganyane ni ngumu kupata nafasi.

Wasanii wenye faida ni wale ambao wananyimbo zinazofanya vizuri miezi kadhaa kabla kwa mfano kuna wasanii ambao walikuwa na nyimbo zinafanya vizuri toka mwaka umeanza au miezi 2 au 3 nyumba naongelea toka mwezi wa 3 na wa 4 mpaka sasa hao ndiyo rahisi kupata namba zao mapema.

Jackson Brown amewahi kusema ” The Best Preparation for Tomorrow is doing Your best today “ ila wasanii  wa Tanzania naona huwa mnasubiri maandalizi ya kesho myafanye kesho hiyo hiyo, Guys you Can?t compete  na mkategemea kushinda na aliyefanya maandalizi jana kwa ajili ya Leo, labda itokee bahati tu.
Na mtaishi kwa bahati mpaka lini?

Kama wasanii huwa mna mwalimu anayewaambia kutoa ngoma kipindi hiki ama kwa hakika mwalimu wenu naye anahitaji mwalimu ili afundishwe tena huenda kuna some important pages aliziruka. Mnachosha tu wasikilizaji kwa kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja wakati mnachokilenga kukipata hamkipati, Kwangu  Huu ni Uwezo mdogo wa kufikiri kwa wasanii wengi wa Tanzania.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY