WAKALA WA WA MBWANA SAMATTA WA GENK AELEZA KAMA MCHEZAJI HUYO ATAONDOKA...

WAKALA WA WA MBWANA SAMATTA WA GENK AELEZA KAMA MCHEZAJI HUYO ATAONDOKA GENK AMA ATABAKI MSIMU HUU

0

Wakala wa mchezaji mtanzania Mbwana Ally Samatta  anayekipiga katika Club ya FC GENK ya  ligi kuu ya Ubelgiji ameelezea kuhusu hatma ya Samatta kama atabaki au ataondoka FC GENK kipindi hiki cha Usajili.

Jamal Kasongo ambaye ndiye wakala wa Samatta amesema Mchezaji huyo hataondoka Klabuni hapo licha ya tetesi za kuhusishwa kuwaniwa na timu kadhaa barani ulaya.

Kasongo ameieleza Kipindi cha Sports leo cha radio one kuwa Samatta bado anahitaji apate uzoefu wa ligi za ulaya kwahiyo bado ataendelea kuwepo Genk angalau kwa mwaka mmoja zaidi, Then mwakani anaweza akaelekea katika club nyingine baada ya kuwa na uzoefu wa kutosha.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY