DEMO
STAMINA AAMUA KUWAPA MAKAVU LIVE WASANII WENZAKE, UNAJUA CHANZO NI NINI?

STAMINA AAMUA KUWAPA MAKAVU LIVE WASANII WENZAKE, UNAJUA CHANZO NI NINI?

0

Huu ndiyo ujumbe aliouandika Stamina kwa wasanii wenzake kupitia mtandao wa Instagram, akiwalaumu kwa tabia yao ya kutopeana tafu hali inayoleta matabaka.

“UJUMBE KWA ARTIST WENZANGU::

tabia ya kutopeana tafu wenyewe kwa wenyewe ndo inaleta matabaka kwenye mziki

Mwenzako ana show sehemu, au ana nyimbo yake mpya anakutumia cover ya wimbo au ya show yake unaipata kabisa ila hutaki kupost tu.
Cha ajabu za wengine ambao ndo unaamini washkaji zako unazipost fresh tu kwa mbwembwe zote.
Mtu mpaka ana namba yako maana yake tayari mnajuana na mna ukaribu pia, hata kama hamna ukaribu ila sababu ni msanii mwenzie we mpe tu support.
Mnasubiri mpaka mtu afariki/afe ndo mnajifanya kupost r. I. P wakati hawezi hata kuona hiyo post yako.
Mnasubiri mpaka mtu awe ameathirika na madawa, au kapigika kimaisha ndo mnajifanya kupost picha au viclip vya video na kujifanya mnahuzunika.
Me nikifa kausha tu usipost maana sitoona wala haitosaidia kama kipindi niko hai hukufanya hvyo.
#UNAFKI TU# “

Kudownload wimbo mpya wa Stamina bonyeza hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY