MO DEWJI AWAUMBUA VIONGOZI WA JUU WA SIMBA

MO DEWJI AWAUMBUA VIONGOZI WA JUU WA SIMBA

0

Mfanyabiashara Tajiri zaidi  mwenye Umri mdogo Afrika Mohamed Dewji Mo, Ameamua Kuwaumbua viongozi wa Simba.

Jana Katika mkutano wa Simba Moja katti ya viongozi wa juu wa Simba alisema Mo hajawafata kutaka kuwekeza katika club hiyo, Mo leo ameibuka na kusema Ameshakutana na Evance Aveva ambaye ni Rais wa Simba mara tatu kujadiliana juu ya jambo hilo.

Mo aliendelea kufunguka kuwa Evance Aveva na Baadhi ya Viongozi wa Simba hawataki Mo Aichukue timu hiyo kwa kumiliki hisa, na hata jana wakati wa kikao walitaka wachengeshe mambo ila nguvu ya wanachama ilifanya suala la Mo Dewji lijadiliwe.

Mo leo mapema amepeleka Barua Rasmi kwa viongozi wa Club ya Simba kueleza azma yake ya kutaka kuwa na hisa katika club hiyo ya mitaa ya msimbazi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY