DEMO
MR. T TOUCH AELEZA SABABU KUU ZA UGOMVI WAKE NA NAY WA...

MR. T TOUCH AELEZA SABABU KUU ZA UGOMVI WAKE NA NAY WA MITEGO

0


Producer Mr. T Touch amefunga sababu kuu iliyofanya yeye na Nay wa Mitego kutokwenda sawa na kusababisha kuachana na Free Nation na Kuamua kufungua studio zake mwenyewe.

Ukiachana na dharau ambao Touch anadai Nay wa Mitego alikuwa nazo, na hali ya Nay kupenda kuwa juu yeye tu huku akimsahau kabisa Producer wake huyo wa hits kibao Touch alisema sababu kubwa iliyomuudhi ni  Pale Nay wa Mitego Alipoacha kwenda kwenye Show yake.

Mr. T Touch akiongea kupitia Top 20 ya clouds fm alisema aliandaa show kwao Songea huku akitumia gharama nyingi kuandaa show hiyo ila cha ajabu Nay Wa Mitego tofauti na Makubaliano yao hakufika kwenye show hiyo.

Touch anadai Nay Alikuwa akimdanganya siku hiyo huku akimwambia anakuja kwenye show kumbe yuko mwanza, Touch akazidi kusema kuwa hata mida ilivyokuwa inazidi kwenda Alikuwa akimpigia simu  basi nay Hakupokea Simu zake, huku akipokea simu ya mtu mwingine ambaye alikuwa eneo moja na Mr T Touch.

Hata Hivyo Mr. T kwake hilo haikuwa sababu ya kuchukia ila kilichomchukiza zaidi ni pale walipokutana Dar na Bado Nay hakuonyeshwa kuguswa juu ya hilo jambo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY