TETESI ZA USAJILI NA HABARI ZA KISOKA MAJUU LEO AUGUST 5 (5/8/2016)...

TETESI ZA USAJILI NA HABARI ZA KISOKA MAJUU LEO AUGUST 5 (5/8/2016) KAMA MAGAZETI YA NJE YALIVYOANDIKA

0

Transfer rumours and paper review – Friday, August 5: Everton plot £63m Draxler move, Pogba to Man United COMPLETE and MORE
KARIBU KATIKA TAARIFA MBALIMBALI ZA KISOKA (TETESI NA HABARI NYINGINE ZA LEO AUGUST 4/2016
  • Everton wamemtangazia kumuongezea mshahara Romelu Lukaku kwa kumlipa pound milioni 135,000 kwa wiki ili kuendelea kuchezea Everton, ikumbukwe Chelsea wamekuwa wakitajwa kumuwania Lukaku (Daily Mirror)
  • Deal ya Pogba na ManchesterUnited unaambiwa imeshakamilika na kinachosubiriwa ni Pogba kurejea kutoka mapumzikoni ili kujiunga na The Red Devils (Manchester Evening News)
  • Real Madrid huenda wakatibua deal ya Manchester City ya kumsajili kiungo wa Bayern Munich David ALABA baada ya kutajwa kuweka Pound million 55.1 kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo (AS)
  • Mabigwa wa nchini Uholanzi Ajax wanatajwa kuwa na mipango ya kumsajili  Muitaliano Mario Balotelli  (Daily Mail)
  • Jurgen Klopp hayuko tayari kumwachia mchezaji Lucas Leiva kuondoka Liverpool mpaka ahakikishe Idara yake ya ulinzi iko vizuri huku akihofia sana watakapokuwa na majeruhi (Liverpool Echo)
  • Arsenal inamipango ya kumsajili mchezaji wa West Brom na mchezaji wa zamani wa Manchester United Jonny Evans (29)  (Daily Mail)
  • Harry Maguire anampango wa kuomba kuhama club yake ya sasa ya Hull City ili kuhama na kwenda Club ya Middlesbrough (Daily Mail)
  • Kasper Schmeichel anadaiwa kuwa yuko katika mpango wa kuongeza mkataba wake na Leicester City kwa mkataba wa miaka mitano zaidi. (espn)
  • Everton wako tayari kutumia pesa zaidi ili kuhakikisha inamsajili mchezaji toka Wolfburg Julian Draxier, Taarifa za ndani zinadai Everton maarufu kama The Toffees wako tayari kutoa Pound million 63 ili mkumsajili kiungo huyo ambaye siku za karibuni alitangaza kutaka kusepa klabuni hapo na Arsenal wanatajwa kumwania kiungo huyo ( The Independent)
  • Mchezaji wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand Amesema Pogba anatakiwa kuletwa kwa kiwango chochote cha Fedha Manchester  United (ESPN)

Usikose kuwa unaembelea www.kwataunit.com kwa habari za michezo na burudani kwa ujumla.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY