UTAFITI: KUNA SIKU DUNIANI HAKUTAKUWA NA VIUMBE HAI KAMA WATU,MIMEA NA WANYAMA...

UTAFITI: KUNA SIKU DUNIANI HAKUTAKUWA NA VIUMBE HAI KAMA WATU,MIMEA NA WANYAMA SOMA ZAIDI

0

Venus might have provided a comfortable place for life – for up to 2 billion years of its early history, according to a new study
Mercury ndiyo sayari iliyokaribu zaidi na Jua ila licha ya hivyo siyo Sayari yenye Joto zaidi, Sayari yenye Joto zaidi ni Venus ambayo ni ya pili kutoka  kwenye jua ambayo Joto lake linakadiriwa kuwa ni 462 C  Kwa kila sehemu ya Sayari hiyo.

Sasa kuna tafiti moja imefanywa na wanasayansi kutokea NASA na kubaini kuwa zamani SAYARI hiyo kulikuwa na uwezekano wa viumbe Kuishi kwenye sayari hiyo yenye Joto zaidi miongoni mwa sayari zote.

Wanasayansi hao wamesema kuwa takribani miaka bilioni na nusu iliyopita inaonekana kulikuwa na maji kwenye sayari ya Venus na Joto lililokuwepo lilikuwa linaruhusu Viumbe hai kuishi, Na inawezekana kulikuwa na Viumbe hai.

Wanasayansi hao pia wametabiri kuwa huenda ipo siku Dunia ambayo ndiyo sayari tunayoishi nayo ikawa haina Viumbe hai kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwasasa Sayari ya Venus ndiyo syari ambayo ni ngumu kiumbe hai kuishi kutokana na kuwa na joto kubwa sana, ukipanga sayari za kiumbe hai kuishi hii inaweza ikawa ya mwisho kabisa maana jiulize Dar Joto huwa halifiki hata Centigrade 40 ila watu wanalalamika je hizo 462 hali Ikoje?


NO COMMENTS

LEAVE A REPLY