GYAN ATAJA VINAVYOMFELISHA SIMBA, ASEMA SASA KILA KITU SHWARI

GYAN ATAJA VINAVYOMFELISHA SIMBA, ASEMA SASA KILA KITU SHWARI

0

Image result for mghana wa simba
STRAIKA wa kimataifa wa timu ya Simba Nicolaus Gyan amefunguka kuwa kutofanya kwake vizuri katika klabu ya Simba kumetokana na mambo kadhaa ambayo yamemfanya kutoona kile ambacho wengi walimtegemea kutokana na CV ya alipotoka.

Gyan amesema alikuwa na matatizo ya kifamilia Nyumbani kwao na pia alikuwa na matatizo yake binafsi Tanzania ila kwasasa yameisha, sababu nyingine msomaji wa Kwataunit.com  ni Ubovu wa Viwanja vingi ambapo Msomaji wa Kwataunit.com vimemfanya kushindwa kucheza vizuri kutoakana na kuwa na pitch Mbovu.

Nimemaliza matatizo yaliyokuwa nyumbani na hata ambayo nilikutana nayo hapa. Kitu kingine ambacho kimechangia kuwa kama hivi ni viwanja vya hapa eneo la kuchezea ni gumu kuliko nilivyozoea kucheza kule kwetu.

Yote kwa Yote kwasasa ameahidi kuwa watu wategemee makipa kuwa wanaokota Mipira nyavuni tu baada ya masuala yote kukaa sawa na yeye kuwa amezoea.

Simba ni timu kubwa yenye presha ya mashabiki, kuliko timu ambayo nilikuwa nikicheza hapo awali, lakini kila kitu nimeshakizoea sasa na kilichobaki mimi kuanza kazi ile ambayo imenileta hapa.

Katika mazoezi ya wiki Hii Gyan ameonekana kuwa mchangamfu huku akijituma kucheza vizuri kiasi cha Makocha Omog na Masoud Kuonekana wazi kuvutiwa na uwezo wake.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY