HABARI MPYA NA NJEMA KUTOKA YANGA MCHANA WA LEO

HABARI MPYA NA NJEMA KUTOKA YANGA MCHANA WA LEO

0

Image result for yanga sc

Mshambuliaji wa Timu ya Yanga ambaye hajaonekana kwenye Kikosi chochote iwe cha kwanza au hata akiba toka msimu umeanza AMIS TAMBWE habari  njema ni kwamba leo ameanza mazoezi rasmi  na wenzake baada ya kufanya mazoezi ya peke yake kwa siku kadhaa.

Tambwe msomaji wa Kwataunit.com wakati wa mazoezi alionekana kuwa mwenye furaha ameonekana kufanya mazoezi vizuri huku akifanaya vyema mazoezi ya kupiga mashuti golini wakati wa mazoezi ya timu ya Yanga yanayofanyika katika uwanja wa Uhuru chini ya Kocha mkuu George Lwandamina.
Image result for amis tambwe 2017
Picha ya Maktaba

Kurejea kwa Tambwe kunaongeza Imani ya Magoli zaidi kwenye Safu ya Ushambuliaji ya Yanga ambayo kwa msimu huu imekuwa ikiwategemea zaidi Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu Migomba.

Kuanza kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake ni dalili kuwa tayari yuko fiti kwa mapambano na huenda Jumamosi Mwalimu Lwandamina akamtumia kuwaangamiza Prisons katika uwanja wa Azam(Azam Complex). Kwa Habari za Michezo za kila siku like Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY