KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA PRISONS LEO 25.11.2017 KINAWEZA KUWA HIVI.

  0  Huu ni Utabiri wa KIKOSI cha Yanga kinachoweza kuanza leo 25 November 2017  dhidi ya Prisons

  Golini kama kawaida ataanza kipa ambaye amekuwa tegemeo zaidi kwa Yanga msimu Huu Youthe Rostand  shavu la Kulia Juma Abdul na Kushoto Gadiel Michael na hii ni kutokana na kufanya vizuri kwa walinzi hawa wa pembeni toka msimu huu umeanza kiasi cha kuwa wachezaji wa kikosi cha kwanza.

  Mabeki wa Kati : Kurejea kwa Kelvin Yondani ambaye alikosekana mchezo uliopita nafikiri kutamrudisha kucheza na Pacha wake msimu huu Andrew Vicent katika eneo la beki wa Kati eneo ambalo kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakicheza kwa kuelewana kiasi,  Katika mchezo uliopita msomaji wa Kwataunit.com Andrew Vicent alisimama na Cannavaro ambaye kurejea kwa Yondani kunaweza kumuweka benchi.

  Viungo : Eneo la katikati ya uwanja Pato Ngonyani anaweza kuendelea kukichafua kama Tshishimbi hatakuwa amepona sawasawa na inaelezwa kuwa bado hajawa fiti asilimia 100 kwahiyo ni nafasi ya Pato tena leo wakati namba 8 Raphael Daudi ITAKUWA ni nafasi yake nyingine kuonyesha kuwa kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City hakubahatisha kuonyesha uwezo mkubwa.

  Winga : Namba saba na kumi na Moja kama kawaida anaweza akaanza Pius Buswita kama Winga namba 7, wakati Winga wa kushoto anaweza akaanza Emmanuel Martin ambaye alipachika bao 2 katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City.

  Washambuliaji : Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib Migomba bila shaka msomaji wa Kwataunit.com  ndiyo watakaoaminiwa zaidi na kuanza katika safu ya Ushambuliaji hasa kutokana na kuelewana kwao katika mechi nyingi wakicheza pamoja huku leo Amis Tambwe anaweza kuingia kwa baadaye kuchukua Sub ya mmoja wao au Kati ya Emmanuel Martin au Buswita mmoja akatolewa kisha Ajib akavutwa pembeni na Kisha Tisa na Kumi wakasimama Chirwa na Tambwe.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY