MANARA Achachamaa Lipuli kuitwa tawi Simba, Aitaja Yanga akijitetea

MANARA Achachamaa Lipuli kuitwa tawi Simba, Aitaja Yanga akijitetea

0

Baada ya kuwepo taarifa za kuwepo Undugu kati ya Simba na Lipuli ya Iringa wengi wakiangalia benchi la Ufundi la Lipuli ambalo linaongozwa na Amri Said pamoja na Suleiman Matola huku baadhi ya washabiki wakibeza mechi kati ya Lipuli na Simba kuwa Simba atajichukulia Points 3 bila Ubishi kutokana na benchi lote kuwa la Simba Haji Manara atolea Ufafanuzi.

Akiongea na EFM Haji amekataa kujibu taarifa ambazo zimekuwa zikizuka tu mitandaoni huku akisema suala la Simba kutajwa kuwa na Undugu na Lipuli kisa Amri Said basi watu wanaosema hivyo wahoji pia Kuhusu Afisa habari wa YANGA Dismas Ten kwenda Yanga akitoka kuwa msemaji wa Mbeya City.


Mbona Dismas Ten ametoka Mbeya City kwenda Yanga hamuulizi mnauliza la Amri Said Tu? Mbona hilo hamuulizi, mi najua majawabu yake yapo Mnauliza Swali na mimi nakupa swali he Kwaheri 

Simba msomaji wa Kwataunit.com itacheza na Lipuli katika mchezo wake unaofuata katika uwanja wa Chamazi siku  ya Jumapili 26.11.2017 wakati Yanga watashuka Dimbani Jumamosi kucheza na Prisons katika uwanja huo huo wa chamazi. Kwa habari za Uhakika za Kila siku like Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY