MPYA : HABARI MPYA 2 KUTOKA YANGA MCHANA WA LEO

MPYA : HABARI MPYA 2 KUTOKA YANGA MCHANA WA LEO

0

KAMUSOKO, TSHISHIMBI WAKOSA MAZOEZI YA LEO.

VIUNGO wa kimataifa wa Klabu ya Yanga Thaban  Kamusoko na Papy Kabamba Tshishimbi wameendelea kukosekana katika mazoezi ya klabu ya Yanga ambayo yameendelea leo, Kamusoko na Tshishimbi walitokea katika mazoezi lakini wakawa watazamaji tu wa mazoezi ya wachezaji wenzao.

Kamusoko alitonesha goti lake hali inayomfanya kuendelea kukaa benchi na akishindwa kufanya mazoezi akisubiri kuimarika zaidi kabla ya kuanza mazoezi ya Nguvu na wenzake.
Tshishimbi ambaye yeye hasumbuliwi na majeruhi bali anaumwa Malaria hali iliyomfanya akose mchezo kati ya Yanga na Mbeya City Jumapili, mchezo ulioisha kwa Yanga kushinda bao 5 kwa 0. ZISOME HABARI ZAIDI ZA YANGA >> BONYEZA HAPA <<
NGOMA BADO PASUA KICHWA YANGA
Mchezaji wa kimataifa wa Yanga kutokea Zimbabwe Donald Ngoma amezidi kuwa pasua Kichwa katika klabu hiyo mara baada ya kudaiwa kuwa bado yupo kwao Zimbabwe ambapo anadaiwa alikwenda kwaajili ya matibabu licha ya Uongozi wa Timu hiyo kusema kuwa Ngoma hakuwaaga na Akirudi basi Adhabu lazima Imhusu.
Donald Ngoma msomaji wa Kwataunit.com amekosa michezo kadhaa ya Ligi kutokana na kuwa majeruhi na amekuwa hayupo nchini kwa wiki kadhaa sasa akidaiwa kuwa kwao nchini Zimbabwe, Kuna taarifa za chini chini kuwa Yanga huenda wakaachana naye wakati wa dirisha dogo kama mambo yataenda sawa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY