NGOMA NA YANGA WAFIKIANA PABAYA, HILI LINAWEZA KUTOKEA WOWOTE

NGOMA NA YANGA WAFIKIANA PABAYA, HILI LINAWEZA KUTOKEA WOWOTE

0

Image result for DONALD NGOMA 2017

Klabu ya Yanga na Mchezaji wake Mzimbabwe Donald Ngoma inaelezwa kuwa hali imefikia katika hatua mbaya zaidi mara baada ya makubaliano ambayo waliyaweka kati ya Ngoma na Uongozi wa Yanga kuelekea Kufika wakati ambao hakuna dalili za Ngoma Kutimiza makubaliano hayo.

Inadaiwa kuwa Ngoma aliambiwa na Uongozi kuwa kufikia tarehe 24 Novemba siku ya leo  basi awe ameripoti katika Klabu hiyo inayotokea mitaa ya Twiga na Jangwani kwaajili ya Kupewa Utaratibu na endapo atakuwa hajafika basi Atasimamishwa klabuni hapo.

Taarifa za Ndani kutoka Yanga zinadai kuwa Endapo Ngoma atasimamishwa basi suala lake litaamuliwa na Kamati ya Nidhamu ya Klabu hiyo na kuna uwezekano kama kamati haitaridhishwa na Utetezi wake basi anaweza akafukuzwa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY