SABABU YATAJWA MBEYA CITY KUPIGWA 5 NA YANGA, VIONGOZI WANENA HAYA

SABABU YATAJWA MBEYA CITY KUPIGWA 5 NA YANGA, VIONGOZI WANENA HAYA

0

Mara baada ya Mbeya City kupigwa goli 5 kwa 0 aka Khamsa (Kiarabu) na mabingwa wa Soka Nchini Klabu ya Yanga imesemekana kuwa sababu ya wachezaji kucheza chini ya Kiwango ilikuwa ni sababu ya madai ya mshahara.

Inasemekana wachezaji wa Mbeya City hawakuwa wamelipwa mishahara yao kutoka kwa Uongozi wa Timu hiyo wenye makao yake Makuu jijini Mbeya.

Hata hivyo Kwataunit.com uliutafuta Uongozi wa Klabu ya Mbeya City ili kujua kama taarifa hizo ni za kweli ama za Uongo.

Afisa ahabari wa Mbeya City Shah Mjanja alikanusha taarifa hizo na kusema

Ni matokeo tu haya, hayachagizwi na mishahara, ugomvi au Vita, mambo ya mshahara sio sababu ya timu kufungwa na hakuna shida hiyo ya mishahara, wachezaji wote wako katika hali nzuri timu ilikuwa camp mahitaji yote timu ilihitaji ilipewa niseme matokeo yamekuwa si mazuri siku hazifanani na hizi mechi zimekuwa ngumu pia, amesema Mjanja.

Mbeya City IMEKUWA si timu inayoisumbua Yanga hasa ikicheza JIJINI Dar Es Salaam na mara zote imkuwa ikipoteza ikutanapo na Yanga. Maana imewahi Kuambulia points 4 pekee kwenye misimu 5 toka Ianze kucheza VPL, Point 1 ikipata msimu wa Kwanza ilipopanda Ligi kuu uwanja wa Sokoine na Kushinda mechi moja msimu wa Mwaka 2016/2017 uwanja wa SOKOINE pia.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY