TETESI ZA USAJILI: AJIBU WA YANGA ANATAJWA KUTIMKIA HUKU

TETESI ZA USAJILI: AJIBU WA YANGA ANATAJWA KUTIMKIA HUKU

0
Image result for Misfer Al Farhan

Kuna taarifa kuwa tayari waarabu wamejipanga kutua  nchini kwaajili ya kufanya mazungumzo na Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajibu Migomba ili mchezaji huyo ajiunge na klabu ya Zamalek ya nchini Misri.

Wakala maarufu wa Kikosi cha Zamalek Misfer Al Farhan anatarajiwa kutua nchini mwanzoni mwa mwezi wa 12 (December) kwaajili ya Kuanza Mazungumzo na Ajibu pamoja na Yanga lengo likiwa ni kumsaini mchezaji huyo Fundi wa Kuuchezea mpira awapo uwanjani.
Zamalek msomaji wa Kwataunit.com  wametenga kiasi cha Euro 50,000 zaidi ya Milioni 130 za kitanzania kwaajili ya Kumalizana na Ibrahim Ajib na hiyo ni pesa ya mchezaji pekee na Klabu itakula pesa zake kivyake nje ya Milioni 130.
Kulingana na wakala Misfer Al Farhan amedai wameanza kumfatilia Ajibu toka alipokuwa Simba na kwasasa amezidi kuwavutia kutokana na kiwango bora anachoonyesha akiwa Yanga na ndipo benchi la Ufundi likaagiza kuwa mchezaji huyo ni muhimu kutua kwenye kikosi cha Zamalek . Kumbuka kulike Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY