USAJILI : SASA SIMBA WASHINDWE WENYEWE TU KUMSAJILI STRAIKA HUYU

USAJILI : SASA SIMBA WASHINDWE WENYEWE TU KUMSAJILI STRAIKA HUYU

0

Image result for walter bwalya
Mara baada ya kocha Mkuu wa Azam Fc  Aristica Cioaba Kusema Mghana Atapendeza zaidi wakati ambao alitaka kusajiliwa mmoja kati ya mastraika wawili mmoja kutoka Ghana na Mwingine kutoka Zambia huku moja kati ya Majina yaliyotajwa kuhitajika na Azam Fc likiwepo jina la Walter Bwalya jina ambalo limekuwa likitajwa na Upande wa Simba, Mambo yanaweza yakawa mepesi kwa Simba kumnasa Mzambia Huyo mara baada ya Azam kukamilisha usajili wa Mghana Benard Arthur.

Benard akisaini Azam Fc hapo jana

Kama Azam wangekomaa na Walter Bwalya basi kungekuwa na ushindani na Simba lakini kwakuwa tayari Azam wameshamalizana na Mghana basi msomaji wa Kwataunit.com  kazi huenda ikawa nyepesi zaidi kwa Simba kumshawishi straiker huyo Wa Zambia Kutua ndani ya Simba.

Lakini mara kadhaa Msemaji wa Klabu ya Simba amenukuliwa akisema wanasubiri Ripoti ya Kocha Mkuu Joseph Omog ili waweze kukamilisha suala la Usajili na hawatasajili mchezaji bila matakwa ya Mwalimu Omog.Kwa tetesi za Usajili za Kila siku like Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY