YANGA : HAWA WATATU SIYO MAJERUHI ILA LEO HAWATAKUWEPO HATA BENCHI

YANGA : HAWA WATATU SIYO MAJERUHI ILA LEO HAWATAKUWEPO HATA BENCHI

0

Wachezaji Haji Mwinyi Mgwali, Abdallah Shaibu Ninja na Matheo Anthony ambaye amenyoa Rasta zake siku za karibuni watakosekana katika Mchezo wa Yanga dhidi ya Prisons leo na Hii ni kutokana na wachezaji hao kujiunga kwenye kambi ya Timu ya Taifa ya Zanzibar inayojiandaa na michuano ya CECAFA Senior challenge Cup inayotarajiwa kufanyika nchini Kenye December mwanzoni.

Wachezaji hao msomaji wa kwataunit.com wanaonekana kutokuwa na nafasi katika kikosi cha Mwalimu George Lwandamina na ndiyo sababu Benchi la ufundi limeamua kuwaruhusu, Unaweza ukahoji upande wa namba 3 kama Gadiel Akiumia nani atacheza lakini Mwalimu George Lwandamina msimu uliopita aliwahi kumtumia Geofrey Mwashiuya kama namba 3.

Upande wa Ninja  msomaji wa Kwataunit.com Cannavaro anaweza kuwa Replacement yake wakati Matheo Anthony ni wazi hana nafasi mara baada ya Amis Joslyn Tambwe kurejea licha ya kuwa ni wazi itakuwa Ngumu kupata nafasi asilimia 100 katika mchezo wa leo, anaweza kupata nafasi kipindi cha pili.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY