Hii ndiyo Changamoto Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Mbeya City

Hii ndiyo Changamoto Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Mbeya City

0

Hii ndiyo Changamoto Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Mbeya City

Wakati baadhi ya wachezaji wakiwa wamejihakikishia namba ndani ya Kikosi cha Simba kwa siku za Karibuni wengine wamekuwa kwenye wakati mgumu kuendelea kutetea namba zao kwenye Kikosi.

> Habari za Simba soma hapa <<

 

Wachezaji kama Aishi Manula, Nicolas Gyan, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Bocco, Erasto Nyoni, Okwi na Shomari Kapombe wao wamekuwa Na Uhakika wa Kuanza kwenye Kikosi cha Kwanza.

Moja ya changamoto ambayo inaweza ikatoea kwenye Kikosi cha Simba leo ni eneo la Mabeki wa Kati.

Kuna juuko Murshid, Erasto Nyoni, Yusuph Mlipili, Salim Mbonde ambaye naye ameanza Kurejea Kikosini baada ya Kuwa majeruhi, na Kijana Paul Bukaba ambaye kwenye mchezo uliopita aliupiga Mwingi kiasi cha kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Simba.

Katika Mchezo wa leo Benchi la Ufundi la Simba linaweza likawa linaumia namna ya kupanga wachezaji hao katika kikosi cha Kwanza.

Katika mechi kadhaa zilizopita msomaji wa Kwataunit Kocha Pierre Lechantre aliweza kumudu kuwaanzisha mabeki watatu wenye asili ya Kucheza kama mabeki wa kati kwa pamoja yani Erasto Nyoni, Juuko na Mlipili kwa Pamoja.

Sasa Ongezeko la Paul Bukaba na Ubora aliouonyesha katika mchezo Uliopita Simba ikipata Ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar,  leo utafanya vichwa Vigonge nani aanze nani abaki kwanza.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY