Matokeo Ruvu Shooting vs Azam Fc 13 April 2018

Matokeo Ruvu Shooting vs Azam Fc 13 April 2018

0

Matokeo Ruvu Shooting vs Azam Fc 13 April 2018

Matokeo kati ya Ruvu Shooting wakiwa wenyeji wa Azam Fc mechi ikichezwa katika uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

Mwamuzi wa Kati ni Shomari Lawi.

Timu ziko uwanjani wakati wowote Mechi itaanza

Mechi imeanza katika uwanja wa Mabatini

Ruvu 0 – 0 Azam Fc

Dakika ya Kwanza Azam Fc wanapata Kona

Dakika ya Pili Inapigwa Kona MABEKI Wa Ruvu Shooting wanaosha na Kuondoa mpira katika Hatari

Dakika ya 7 Shaaban Msala alijaribu kuondoka na Mpira na Kupiga Shuti linalokwenda Nje ya Lango

Ruvu Shooting 0 – 0 Azam Fc

Ruvu Shooting wanaonekana kucheza Vizuri zaidi ya Azam Fc katika dakika 10 za Mwanzo wakipiga pasi Fupi na Kujaribu kutengeneza Mashambulizi.

Dakika ya 13

Ruvu Shooting 0 – 0 Azam Fc

Dakika ya 14 Bryson Raphael wa Azam anaonekana kuumia na Huenda akashindwa Kuendelea na pambano

Ruvu Shooting wanakosa bao katika dakika ya 17 Almanusra Azam Wajifunge

Ruvu Shooting 0 – 0 Azam

Dakika ya 20 Amani George wa Ruvu anaondoka vizuri na Mpira akiwa amebaki na Kipa anapiga Nje

Bryson Raphael anaonekana kurejea uwanjani baada ya Matibabu

Dakika ya 24 Kwa mara nyingine Ruvu wanakosa nafasi ya wazi

Dakika ya 28 Hamis Mcha anaipatia goli Ruvu Shooting kwa Mpira wa Adhabu baada ya Bao anaonekana kuomba Msamaha kwani amewahi kucheza katika klabu ya Azam Fc

Ruvu Shooting 1 – 0 Azam Fc

Washabiki wa Ruvu Shooting vijana wa JKT wanaonekana kuzunguka uwanja wakishangilia toka mechi imeanza lakini baada ya Goli morali ndiyo imezidi’

Dakika ya 33

Ruvu Shooting 1 – 0 Azam Fc

Dakika ya 40 Salum Aboubakary anatengeneza nafasi nzuri kwa Benard Arthur lakini mpira unapaa sentimita Chache kwenda Juu

Ruvu Shooting 1 – 0 Azam Fc

Dakika ya 42 Yahya Zayd anapewa kadi ya Njano kwa Kumchezea faulo Damas Makwaya wa Ruvu Shooting

Dakika ya 43 Azam wanashambulia wanapata Kona

Kona inazaa kona Nyingine lakini hakuna matokeo Chanya kwa Azam Fc, Bado wako nyuma kwa Bao 1

Half TIME

Ruvu Shooting 1 – 0 Azam Fc (Hamis Mcha)

KIPINDI CHA PILI

Dakika ya 48

Ruvu 1 – 0 Azam Fc

Dakika ya 50 Azam wanakosa nafasi ya Wazi Kipa anapangua mabeki wanatoa na kuwa Kona

Mpira umeng’ang’ania Langoni mwa Ruvu

Azam wanapata kona katika dakika ya 55.

Inapigwa kona Fupi lakini mabeki wa Ruvu wanaonekana kuruka Juu zaidi ya washambuliaji wa Azam na kuokoa Mpira

Dakika ya 57 Benard Arthur anapiga kichwa mpira unagonga mwamba wa Juu Kipa anadaka

Ruvu 1 – 0 Azam

Dakika ya 63 Mbaraka Yusuph anaingia kuchukua nafasi ya Joseph Mahundi

Dakika ya 70 bado Mambo magumu kwa Azam wako nyuma kwa bao 1 kwa 0

Dakika ya 70 mfungaji wa Goli la Ruvu Hamis Mcha anatoka nafasi yake anaingia Jamal Soud

Dakika ya ya 75 Aggrey Moris anapewa kadi nyekundu na Kutolewa Nje ya uwanja mara baada ya Kumchezea Kipepsi mchezaji wa Ruvu

Dakika ya 80 Ruvu Shooting wanapata Bao la Pili kupitia kwa Full Zulu Maganga

Ruvu 2 – 0 Azam Fc

Zimeongezwa dakika 4 za Nyongeza

Ruvu 2 – 0 Azam Fc

Dakika 90 zimeisha

FULL TIME

Ruvu Shooting 2 – 0 Azam Fc (Hamis Mcha, Fuluzulu Maganga)

SHUKA CHINI KUSOMA ZAIDI HABARI ZETU

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY