Matokeo Simba vs Mbeya City 12 April 2018

Matokeo Simba vs Mbeya City 12 April 2018

0

Matokeo Simba vs Mbeya City 12 April 2018

Matokeo Kati ya Simba dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Taifa Jijini  Dar Es Salaam, kwataunit.com Tunakupa Matokeo ya Moja kwa moja 

> Soma habari zaidi za Michezo <<

Timu zinasalimiana tayari kwa Pambano kuanza

Mwamuzi wa Mchezo wa Leo ni HANCE MABENA

Mechi im eanza Katika uwanja wa Taifa

Simba 0 – 0 Mbeya City

Dakika ya 2 Simba wanapata Kona, Inapigwa Kona Fupi, Simba wanatengeneza Shambulizi lakini wachezaji watatu wanaenda katika mpira inakuwa ni offside

Dakika ya 4 Emmanuel Okwi anawekwa Chini karibu na kumi na nane, Inapigwa Faulo mabeki wanaokoa

Dakika ya 6 Babu Ally anapewa kadi ya njano baada ya kumwingilia vibaya Jonas Mkude

Simba 0 – 0 Mbeya City

Dakika ya 10 Victor Hangaya anajaribu shuti kipa Manula anacheza mpira Ule

Simba 0 – 0 Mbeya City

Dakika ya 13 Okwi anawekwa chini na walinzi wa Mbeya City, Faulo kuelekea Mbeya City

Dakika ya 14 Inapigwa Faulo na Mkude lakini Mabeki wanaokoa

Dakika ya 14 Bocco anapiga Krosi, Okwi anaugusa kwa Kichwa Kichuya anachelewa, Goal Kick

Goooooal dakika ya 16 Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao la Kwanza, Alipiga Bocco kipa Owen Chaima akapangua mpira ukawa unaambaambaa Ukakutana na Okwi ambaye anafanya kazi nyepesi tu ya Kuuweka Nyavuni

Simba 1 – 0 Mbeya City

Dakika ya 20

Simba 1 – 0 Mbeya City

Dakika ya 23 Eliud Ambokile anajaribu shuti la Mbali lakini mpira uanenda Nje ya Lango

Dakika ya 25

Simba 1 – 0 Mbeya City (16′ Emmanuel Okwi)

Dakika ya 29 ilichezwa Kaunta, Okwi akamtangulizia Bocco lakini Bocco anasogea na Kupiga Nje.

Dakika ya 31 inapigwa Kona fupi na Simba, Walinzi wa Mbeya City wakidhani ameotea Asante Kwasi anaipatia Simba bao la Pili, Ni Assist ya Shiza Kichuya.

Owen Chaima anapewa kadi ya Njano kwa kumlalamikia kadi

Simba 2 – 0 Mbeya City

Dakika ya 33 Frank IKobela anaipatia Mbeya City bao akitumia vizuri mpira wa Kona akipiga kwa Kichwa.

Simba 2 – 1 Mbeya City

Dakika ya 34 John Bocco anafunga bao la 3 kwa Simba

Simba 3 – 1 Mbeya City

Dakika ya 37 Frank Ikobela anaonekana kuwa hatari zaidi kwa walinzi wa Simba mpaka sasa.

Simba 3 – 1 Mbeya City

Dakika ya 38 Kona upande wa Mbeya City wanapiga, kapombe anatoa na kuwa kona Nyingine, Inapigwa Inakuwa Kona Nyingine.

Inapigwa kona mabeki wa Simba wanaosha

Dakika ya 42 Ally Lundenga anapewa kadi ya Njano baada ya Kumzuia Okwi.

Dakika ya 43 Hamid Mohammed anaingia kuchukua nafasi ya Babu Ally

HALF TIME

Simba 3 – 1 Mbeya City (Okwi,Kwasi,Bocco, Frank Ikobela)

kipindi cha pili kimeanza

Simba  3 – 1 Mbeya City

Dakika ya 46 Simba wanashindwa kuweka Mpira kambani Okwi anakata tamaa ya Kuufata  Mpira

Dakika ya 50 Mbeya City wanaanza kwa Kutulia kipindi cha Pili lakini safu ya Ulinzi ya Simba inaonekana kuwa makini na Kuosha mashambulizi

Simba  3 – 1 Mbeya City

Dakika ya 53 Okwi anatelezeshewa Mpira na Bocco, Okwi anatandika Bakora mpira Unagonga mwamba wa Juu na Kurudi uwanjani.

Dakika ya 57  Shiza Kichuya anawakosa Mbeya City, Owen Chaima anakuwa Shujaa kwa Kuutoa mpira na Kuwa Kona

Simba 3 – 1 Mbeya City (Okwi,Kwasi, Bocco)

Dakika ya 58 Inapigwa kona na Shomari Kapombe Owen Chaima anautoa Mpira kwa Punch wakati huo anamuumiza Asante Kwasi ambaye Yupo chini

Dakika ya 60 Danny Joram anatoka kumpisha Mohammed Samatta

Dakika ya 64 shuti la Mbali lililopigwa na Emmanuel Okwi linakosa Nguvu

Dakika ya 65 KROSI safi ya Victor Hangaya inapigwa kichwa na NA Frank Ikobela Manula anaruka kama Nyani na Kuudaka

Simba 3 – 1 Mbeya City

Dakika ya 66 Ramadhan Malima anamwangusha Shiza Kichuya ni mpira wa Adhabu kuelekea Mbeya City, Okwi anapiga mpira Unambabatiza Mohammed Samatta

Dakika ya 70

Simba 3 – 1 Mbeya City

Dakika ya 73 Mohammed anaingia Kuchukua nafasi ya Kwasi ambaye ameumia na kushindwa kuendelea na Pambano

Dakika ya 74 Frank Ikobela anamburuza Chini Mohammed Hussein na Anapewa kadi ya Njano na Mwamuzi Hance Mabena

Dakika ya 76 Hangaya anatoka anaingia Geofrey Milla

Simba 3 – 1 Mbeya City (Okwi, Kwasi, Bocco – Ikobela)

Dakika ya 79 Bocco anatoka anaingia Laudit Mavugo kwa Upande wa Simba.

Dakika ya 83 Mbeya City wanapata Kona hata hivyo inashindwa Kuzaa bao.

Dakika ya 84 Mbeya City wanapata kona nyingine, Wanapiga lakini wanaambulia Patupu

Simba 3 – 1 Mbeya City(Okwi,Kwasi, Bocco)

Dakika ya 87 anaingia James Kotei anaToka Nicolas Gyan

Dakika mbili za Nyongeza ndizo zimebaki kuamua

Katika za Mwisho Okwi, Mkude wanawakosa tena Mbeya City

Mpira Umekwisha katika uwanjwa wa taifa

Simba 3 – 1 Mbeya City.. Tembelea Kwataunit.com Kila siku kwa Habari za Michezo wakati wote

SHUKA CHINI KUSOMA ZAIDI HABARI ZETU

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY