Matokeo Yanga vs Singida United VPL 11 April 2018

Matokeo Yanga vs Singida United VPL 11 April 2018

0

Matokeo Yanga vs Singida United VPL 11 April 2018

Matokeo mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League yanga na Singida United.

Soma habari za Michezo hapa <<

Kuanzia saa kumi kamili Tutakuwekea Matokeo ya Moja kwa Moja (Live Updates)

Timu zinatoka vyumbani tayari kwaajili ya Kusalimiana na Mgeni Rasmi

Jacob Adongo ndiye mwamuzi wa Kati katika mchezo wa Leo

Mpira umeanza katika uwanja wa Taifa

Yanga 0 – 0 Singida United

Singida bado wanapiga pasi nyingi katika eneo leo

Dakika ya kwanza Tu Papy Kambale anaipatia Singida bao la kuongoza

Yanga 0 – 1 Singida United

Dakika ya 5 Raphael Daudi anapiga Mpira Unapaa juu ya Lango

Yanga 0 – 1 Singida

Singida bado wanaonekana kuonana zaidi kwa dakika hizi za Mwanzo.

Dakika ya 11 Mhilu anagongana na Ally  Mustapha kipa wa Singida United wakiwania Mpira wa Juu Uliopigwa na Ibrahim Ajibu Kiufundi, Barthez yupo chini

Dakika ya 13 Ally Mustapha ananyanyuka baada ya Kutibiwa pambano Linaendelea

Dakika ya 13 Yusuph Mhilu anapenyeza Mpira kwa Ibrahim Ajibu lakini unakuwa mrefu kwa Ajibu.

Dakika ya 15 Yanga wanapata Kona, Inapigwa inazaa Kona Nyingine lakini Ninja anacheza Faulo

Dakika ya 16 Aliondoka Raphael Daud akapiga kwa Mhilu, Mhilu anapiga shuti beki anatoa inakuwa Kona ilikuwa Hatari sana

Kona Inashindwa kuwa na Madhara, Singida wanaendelea kuzipiga Pasi nyingi katika eneo lao

Dakika ya 20

Yanga 0 – 1 Singida United

Dakika ya 21 Kigi Makasi yupo chini baada ya Kukanyagwa na Hassan Kessy mwamuzi alipeta

Dakika ya 23 Papy Tshishimbi anafanya moja ya jaribio zuri anapiga Shuti linaloenda Kupiga katika shavu la Goli

Yanga 0 – 1 Yanga

Dakika 28 zimekatika mpaka sasa Yanga wakiwa NYUMA kwa bao 1 kwa 0 bao likipatikana dakika ya Kwanza Kupitia kwa Papy Kambale

Dakika ya 29 Ilipigwa krosi ikakutana na Nizar Khalfan ambaye anapiga Shuti linalopaa Juu

Dakika ya 31 Singida wanapata Kona ya kwanza wakati huo Yanga wanakona Nne

Dakika ya 35

Yanga 0 – 1 Singida United (Dakika ya 1 Kambale)

Dakika ya 38 Ally Mustapha anashindwa kuendelea na Pambano anaingia Manyika Jr.

Dakika ya 39 Raphael Daudi  anajaribu kunyoosha na Mguu wa kushoto mpira unapaa juu kidogo ya Lango

Dakika ya 42 Salum Chuku anaingia Kuchukua nafasi ya Batambuze anayeshindwa kuendelea na Pambano baada ya Kuumia, Yanga 0 – 1 Singida United

Ilimiminwa krosi safi na Haji Mwinyi Chirwa akapiga kichwa Kikali, Kipa anapangua beki anatoa inakuwa Kona.

Dakika ya 45 Goaaaaaaaaaal Abdallah Shaibu Ninja anafunga goli kwa Kichwa kona ya Ajibu.

Yanga 1 – 1 Singida United

Mpira Ni Mapumziko katika uwanja wa Taifa

Yanga 1 – 1 Singida United (1′ Kambale, 45′ Ninja)

KIPINDI CHA PILI

Yanga katika dakika ya kwanza Kipindi cha Pili Mhilu alitaka kwenda Kumsalimia Manyika lakini tayari ni Offside

Dakika ya 50 Yanga wanatengeneza Shambulizi inakuwa Kona

Kona inashindwa kuleta Bao

Dakika ya 52 Singida wanapata Kona, Inapigwa Kona fupi lakini mipango inafeli mapema Tu

Yanga 1 – 1 Singida United

Dakika ya 53 Kaseke anaondoka na Mpira Vizuri lakini anapiga Nje, Mashabiki wanamzomea

Dakika ya 57 Chirwa anaiomba anapigiwa na Buswita lakini anaikatia tamaa pasi Hiyo baada ya Kuona ni ndefu

Dakika ya 63 Baada ya Gonga mbili tatu Ajibu anapiga shuti mpira unapaa

Yanga 1 – 1 Singida United

Dakika ya 64 Chirwa akielekea Kumsabahi Manyika Anasukumwa na Kennedy Juma refa anasema hakuna Penati

Dakika ya 66 Chirwa anapewa mpira na Buswita anakosa goli la wazi baada ya Kuzidisha kuupaka rangi mpira, Ilikuwa nafasi nzuri kwa Yanga

Dakika ya 68 Chirwa anajaribu shuti nje ya 18, Kipa anatoa inakuwa Kona

Wakati huo Singida anatoka Nizar Khalfan anaingia Yusuph Kagoma

Dakika ya 70

Yanga 1 – 1 Singida United

Dakika ya 73 anatoka Pius Buswita anaingia Juma Mahadhi

Dakika ya 77 Deus Kaseke anapewa kadi ya Njano baada ya Kuutanguliza Mpira kwa Mkono.

Yanga 1 – 1 Singida United

Mwashiuya Kaingia kuchukua nafasi ya Ibrahim Ajibu

Dakika ya 84 Yusuph Mhilu anamwekea pasi ya Upendo Chirwa, Chirwa anatungua nazi, Anapiga Juu

Dakika ya 87 Hassan kessy anapewa kadi ya Njano

Dakika ya 89 Anatoka Chirwa anaingia Emmanuel Martin

Wakati huo zimeongezwa dakika 3, Kuna mchezaji wa Singida United yupo chini

DAKIKA 90 ZIMEISHA

Yanga 0 – 0 Singida United

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY