Peter Crouch anogesha Goli la Cristiano Ronaldo baada ya Kuandika haya

  0

  Peter Crouch anogesha Goli la Cristiano Ronaldo baada ya Kuandika haya

  Jana Cristiano Ronaldo alifanikiwa Kuiongoza Real Madrid kupata ushindi wa Bao 3 Kwa 0 Real madrid ikiinyuka Juventus waliokuwa Nyumbani huku Ronaldo akifunga mabao mawili.

  Katika mabao aliyoyafunga Goli la Pili ndilo lililokuwa gumzo kutokana na Style aliyoipiga AINA ya Upigaji ukijulikana zaidi kama “Overhead Kick ”

  Lakini baada ya ya goli hilo Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Peter Crouch alizidi kulinogesha bao hilo kupitia Ukurasa wake wa Twitter kwani alikumbushia aina kama ya goli la Ronaldo alilowahi kulifunga akiwa Liverpool walipokuwa wakicheza dhidi ya Galatasaray.

  Kupitia Ukurasa wa Twitter Crouch  msomaji wa Kwataunit.com aliandika  “There is only a few of us who can do that ” akimaanisha

  ” Ni wachache tu kati yetu tunaoweza kufanya hivyo ” 

  Ujumbe huo wa Crouch umekuwa Gumzo mitandaoni na Kufanya watu kuanza Kupambanisha magoli hayo mawili.

  NO COMMENTS

  LEAVE A REPLY