Viwango mechi ya Welayta vimewarudisha hawa Yanga Kikosini

Viwango mechi ya Welayta vimewarudisha hawa Yanga Kikosini

0

Viwango mechi ya Welayta vimewarudisha hawa Yanga Kikosini

Ukikitizama vizuri kikosi cha Yanga utagundua Kuna baadhi ya wachezaji wamerudishwa Kikosini sababu tu ya Kuonyesha Viwango vikubwa katika mechi kati ya Yanga na Welayta Dicha.

Ukianzia eneo la Nyuma mchezaji kama Haji Mwinyi uwezo wake wa Kupiga Majalo yaliyoenda Shule kiasi cha Kuipa Yanga goli la sekunde ya 27 Kocha ameona aendelee kumuamini na Leo.

Abdallah Shaibu “Ninja” Huyu unaweza ukasema amepata nafasi kwakuwa Tu Dante Ameumia lakini Kumbuka alipokuwa akikosekana Dante hata Makapu alikuwa anachukua nafasi ya Kucheza na Yondani.

Kwahiyo naye uwezo mkubwa kwenye mechi dhidi ya Welayta umempa Ulaji wa kuanza Leo.

Katikati ya Uwanja : Pius Buswita kama ulimuangalia vizuri katika mchezo uliopita Buswita alicheza kama namba 8 huku Kamusoko akcheza kama namba 6, Buswita alicheza vizuri sana akiunganisha vizuri timu kwa Kupokea pasi kutoka eneo la Nyumba na kuzipeleka mbele kwa Ustadi Mkubwa leo ameendelea kuaminiwa katika Eneo hilo licha ya Kuwa katika mechi nyingi alikuwa akicheza kama mshambuliaji.

Raphael Daudi Loth huyu msomaji wa Kwataunit Mechi ya Welayta Dicha alicheza kama namba 10 na Kuonekana wazi kubadilika alikuwa mwepesi sana tofauti na Tulivyomzoea katika mechi kadhaa akivaa uzi wa Yang, alipiga pasi nyingi za Uhakika, Kasi kiasi cha kuwa mchezaji hatari akifunga pia bao la mapema, Leo ameendlea Kuaminiwa.

Wengine wanaendelea Kutumikia nafasi zao na wamekuwa wakiaminiwa hata katika mechi Nyingine yaani wao walikuwa wanauhakika wa kuanza, ila hawa niliochambua Viwango vikubwa kwenye mechi ya Welayta vimewafanya waendelee kucheza  na Leo.

Like Ukurasa wetu wa Facebook hapa kama bado >>  bonyeza hapa <<

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY