Wachezaji hatari wa Kuchungwa Lipuli Fc kuelekea mchezo na Simba

Wachezaji hatari wa Kuchungwa Lipuli Fc kuelekea mchezo na Simba

0

Wachezaji hatari wa Kuchungwa Lipuli Fc kuelekea mchezo na Simba

Simba leo watashuka Dimbani kwenye Ardhi ya Mkwawa Iringa Kumenyana na Timu ya Lipuli mchezo wa Ligi Kuu soka ya Tanzania Bara VPL.

Kuelekea Mchezo Huo kuna Wachezaji wa Lipuli ambao ni hatari kwa Upande wa Simba na wanaweza kuwa kikwazo kwa Simba Kupata Ushindi.

Novaty Lufunga

Huyu aliwahi Kucheza Simba na Kwasasa Yupo Lipuli Fc anacheza nafasi ya Ulinzi kama beki wa kati na mara nyingine amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji akiwa Lipuli.

Uzoefu wake wa Kucheza mechi kubwa, Uzoefu wa Kujua wachezaji wa Simba nayo ni faida nyingine kwa Lipuli.

Jamal Simba Mnyate.

Huyu naye aliwahi kupita Simba akiwa kwenye Kiwango bora kabla ya Kupata Majeruhi na UWEZO wake kuonekana kupungua, Huyu naye anaijua Simba na atataka kuonyesha kuwa bado yupo kwenye Ubora wake uleule.

Malimi Busungu

Aliwahi kupita Yanga na ni moja kati ya wachezaji ambao amewahi Kuifunga Simba akicheza Yanga, toka amejiunga na Lipuli amekuwa akitengeneza magoli mengi na katika mchezo wa Mwisho wa Ligi kuu dhidi ya Singida alifanikiwa Kufunga goli likiwa goli lake la Kwanza.

Malimi Busungu atakuwa na hamu ya kuendelea kufunga magoli kwa Timu yake lakini pia kuifunga Simba kwani alianza kuifunga Simba akiwa Mgambo JKT na Yanga.

Adam Salamba

Huyu msomaji wa kwataunit  ni mmoja kati ya Washambuliaji ambao toka amejiunga na Lipuli kutokea Stand United amekuwa Wamoto sana kwa Makipa, Huyu ndiye mchezaji bora wa Mwezi March ligi Kuu  uwezo wake wa Kufunga Magoli unaweza kumfanya kuwa moja kati ya wachezaji hatari wa Kuwatazama leo.

Joseph Owino

Huyu ndiye baba mwenye nyumba wa Lipuli, Beki wa Kati na Ukisikia Lipuli imemaliza mechi bila Kufungwa Jua wazi moja kati ya watu waliofanya shughuli Kubwa Owino naye atakuwa Ndani.

Ni beki anayecheza kwa Umakini lakini pia kucheza Simba inaweza ikawa sababu kubwa ya kutaka kuwaonyesha waajiri wake wa zamani kuwa bado yuko Fiti.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY