Alichokisema Mohammed Rashid kuhusu Usajili wake Msimu Ujao

Alichokisema Mohammed Rashid kuhusu Usajili wake Msimu Ujao

0

Alichokisema Mohammed Rashid kuhusu Usajili wake Msimu Ujao

Straika wa Kutumainiwa wa Tanzania Prisons ambaye amekuwa akihusishwa kutua Simba jana baada ya mchezo kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Singida United alipata nafasi ya Kuzungumza na Mwandishi wetu kuhusiana na Masuala ya Usajili.

Magazeti ya Michezo May 29 2018

Katika mahojiano Mohammed Rashid aliweza Kujibu maswali sita kutoka kwataunit.com kama ifuatavyo.

Swali : Vipi Mkataba wako na Tanzania Prisons?

” Mkataba  wangu na Prisons  ndiyo unamalizika ”

Swali : Kwakuwa mkataba unamalizika Tukutegemee kwenda Timu gani msimu Ujao?

“Kwa timu yoyote Itakayonihitaji mimi niko tayari Kucheza ”

Swali : Timu Gani ambazo zimeshakufata ?

” Hapo sina jibu na siwezi nikakwambia lakini Ni Timu nyingi ”

Swali : Kama Yanga na Simba wameweka mzigo na Mzigo wa Kueleweka wewe binafsi Utachagua wapi?

” Timu yoyote ile mimi naweza Kufanya Kazi endapo tu tukikaa tukazungumza na Kuelewana ”

Swali :Nafasi yako unaiona wapi zaidi kati ya Kikosi cha Yanga na Kikosi cha Simba?

” Mimi nafasi Yangu popote pale naona naweza Kufiti.”

Swali : Vipi ishu ya Kubaki Prisons unampango wa Kuongeza mkataba?

” Kama viongozi wakinifata tukafanya mazungumzo basi mimi sina shida “

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY