Jonas Mkude ataja ambaye hatamsahau msimu Huu VPL

Jonas Mkude ataja ambaye hatamsahau msimu Huu VPL

0

Jonas Mkude ataja ambaye hatamsahau msimu Huu VPL

Kiungo wa Mabingwa wa Soka Msimu wa 2017/2018 Simba, Jonas erald Mkude amefunguka na Kutaja mtu ambaye hawezi kumsahau msimu Huu.

Jonas Mkude ambaye hakuwa na Msimu Mzuri sana timu ilipokuwa chini ya Makocha Joseph Omog na Mganda Jackson Mayanja kutokana na Kukalia Benchi kwa Muda Mrefu amemtaja Masoud Djuma.

Mkude amemtaja Masoud Djuma kama kocha ambaye hatamsahau kwa Msimu huu kutokana na Kumwamini toka alipobaki na Timu kiasi cha Kumfanya kuwa mchezaji muhimu ndani ya Simba na Kuwa kwenye Kikosi cha kwanza cha  Simba Mpaka sasa.

Mkude anakiri kuwa bila Masoud Djuma alikuwa anaona dalili za Kiwango chake Kuporomoka lakini toka kocha huyo aonyeshe Kumwamini amekuwa kwenye Kiwango bora.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY